Ukumbi wachelewesha kesi kina Mdee kuanza

Muktasari:
Mahakama Kuu Masijala Kuu jijini Dar es Salaam imechelewa kuanza usikilizwaji wa kesi iliyofungulia na wabunge 19 wakipinga uamuzi wa Chadema kufukuzwa isivyo kihalali ikisubili ukumbi mkubwa utakaokidhi idadi ya watu walioudhuria kusikiliza kesi hiyo.
Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masijala Kuu jijini Dar es Salaam imechelewa kuanza usikilizwaji wa kesi iliyofungulia na wabunge 19 wakipinga uamuzi wa Chadema kufukuzwa isivyo kihalali ikisubili ukumbi mkubwa utakaokidhi idadi ya watu walioudhuria kusikiliza kesi hiyo.
Wabunge hao wanapinga uamuzi huo kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review), wakidai walifukuzwa isivyo halali kwa kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa, hivyo wanaiomba mahakama hiyo itengue.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa leo Jumatano, Novemba 9, 2022 mbele ya Jaji Cyprian Mkeha ambapo Mbunge wa viti maalumu, Jesca Kishoa anatarajiwa kuhojiwa na mawakili wa Chadema.
Akitoa tangazo hilo, kiongozi wa jopo la mawakili wa Chadema, Peter Kibatala amedai kutokana na wingi wa watu wanaotaka kusikiliza shauri hilo wamekubaliana usubiliwe mahakama ya wazi iliyokuwa kubwa ambao kuna kesi inaendelea utakaotosheleza watu hao kuingia.
"Tusubiri kwa muda hadi hapo utakapopatikana ukumbi mkubwa wa watu wote kuingia kusikilizwa shauri hili," amedai Kibatara
Wengine watakaoitwa kuhojiwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee; aliyekuwa makamu mwenyekiti Bawacha, Hawa Mwaifunga; aliyekuwa Katibu Bawacha, Grace Tendega na aliyekuwa mweka hazina Bawacha, Esther Matiko. Pia, wamo Ester Bulaya na Cecila Pareso.
Mpaka sasa tayari wabunge wanne wa Viti Maalumu wamehojiwa na mawakili wa Chadema kuhusiana na ushahidi wao waliowasilisha mahakamani hapo kwa njia ya kiapo ni Hawa Mwaifunga, Grace Tendega, Nusrat Hanje na Cecilia Pareso.
Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari zaidi