Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UDBS yaanzisha shahada ya uhasibu, mafuta na gesi

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa UDBS, Dk Ulingeta Mbamba alisema: “Sekta hii haina wataalamu wa kutosha ambao watafanya kazi katika kampuni za mafuta katika fani ya uhasibu na usimamizi wa fedha, ndiyo maana tunasomesha vijana hawa ili waje kusaidia kuandaa na kutengeneza sera za mafuta na mikataba.” Aliongeza: “Wanafunzi walioomba kujiunga na shahada walikuwa 200 na wote walikuwa na sifa na vigezo vinavyohitajika lakini kutokana na chuo kutokuwa na uwezo, imebidi tuchukue 40 tu.”

Dar Es Salaam. Kutokana na kugundulika kwa nishati ya mafuta na gesi nchini, Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), imeanza kutoa Shahada ya Uzamili ya Uhasibu na Usimamizi wa Fedha kupitia sekta ya mafuta na gesi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa UDBS, Dk Ulingeta Mbamba alisema: “Sekta hii haina wataalamu wa kutosha ambao watafanya kazi katika kampuni za mafuta katika fani ya uhasibu na usimamizi wa fedha, ndiyo maana tunasomesha vijana hawa ili waje kusaidia kuandaa na kutengeneza sera za mafuta na mikataba.” Aliongeza: “Wanafunzi walioomba kujiunga na shahada walikuwa 200 na wote walikuwa na sifa na vigezo vinavyohitajika lakini kutokana na chuo kutokuwa na uwezo, imebidi tuchukue 40 tu.”

Dk Mbamba alisema programu hiyo ya miaka miwili itahusisha wanafunzi waliomaliza shahada ya kwanza katika masuala ya fedha na uhasibu na kwamba gharama za masomo kwa mwaka ni Sh8.5milioni kwa mwanafunzi kwa miaka yote miwili.

“Kampuni ya Statoil ya Norway ambayo inajihusisha na utafutaji wa mafuta katika bahari kuu nchini imekubali kufadhili masomo ya shahada hiyo kwa wanafunzi 10 kati ya 40,” alisema.

Alisema wafadhili kutoka Chuo Kikuu cha Biashara cha Stavanger, Norway watakuja nchini kuwafundisha wanafunzi hao.

Alisema watakaomaliza shahada hiyo watapata kazi katika taasisi za umma kwa sababu zinahitaji wataalamu wazuri katika ukadiriaji wa kodi. “Jukumu la vyuo vikuu nchini ni kuwawezesha Watanzania kupata uwezo wa kufanya kazi katika sekta ya mafuta na gesi ambao watasimamia mikataba na kutengeneza sera ya mafuta na gesi.”