Tulia Trust kuwapa 300 bima za afya

Muktasari:
- Bima hizo zinatolewa kwa lengo kuwarahisishia upatikanaji wa huduma ya afya katika vituo vya afya, zahanati na hosptali za Serikali.
Mbeya. Taasisi ya Tulia Trust itakabidhi msaada wa bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (ICHF) kwa kaya zisizojiweza wakiwepo wazee zaidi ya 300 mkoani hapa.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi, Januari 21, 2023 ofisa habari na uhusiano wa taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema kadi hizo zinakabidhiwa Jumanne Januari 24 mwaka huu na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Dk Tulia Ackson.
Amesema lengo la kutoa bima za afya katika makundi hayo ni kusaidia kupata huduma bora za afya pindi wanapopata changamoto za kuhitaji matibabu na kudondoka na hadha wanazokumbana nazo za kuhitaji fedha wakati wa kuhitaji huduma.
Mwakanolo amesema licha ya utoaji wa bima za afya pia wazee walipimwa na kuabinika na tatizo la macho watapatiwa miwani bure ikiwa ni mwendelezo wa tukio la utoaji huduma ya macho lillilofanyika Desemba mwaka,” amesema.
“Ilkumbukwe Desemba mwaka jana zaidi ya wananchi 4,000 walipimwa na kupatiwa miwani bure kupitia moja ya taasisi moja kwa kushirikiana na Tulia Trust na wengine ambao hawakufanikiwa watahudumiwa Januari 24 mwaka huu,” amesema.
Kwa upande wake Meneja wa Tulia Trust, Jackline Boaz amesema kuwa wamelenga katika kundi la wazee kutokana na kuwepo kwa changamoto za kuhitaji matibabu ya Mara kwa mara kutokana na umri mkubwa
“Tumetumia utaratibu wa kuyapata makundi hayo kupitia kwa viongozi wa Serikali za Mitaa ambao ndio wanatambua changamoto za jamii kwenye maeneo yao hivyo tunatatajia kutoa kadi za bima zaidi ya 300,” amesema.
Mmoja wa wanufaika wa msaada huo, Rehema Joel amesema utagusa makundi ya wasiojiweza kiuchumi kwani changamoto kubwa kwa ni suala la kukosa matibabu pindi wanapopata na magonjwa mbalimbali.
“Kama mnavyojua sisi wajane na wazee changamoto kubwa ni magonjwa, kwa hiyo unapopata msaada matibabu kwa kweli tunapunguza siku za kuishi kwa kukosa huduma,” amesema.