Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA kutatua changamoto za wajasiriamali

Meneja Utafiti wa TRA, Saada Alluy akizungumza wakati wa kongamano la wafanyabiashara na wajasiriamali

Muktasari:

  • Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema kupitia kongamano la wajasiriamali linawasaidia kutambua changamoto zinazolikumba kundi hilo.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema kupitia jukwaa la kongamano la wafanyabiashara na wajasiriamali lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam watafahamu changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo na wa kati na kuzitafutia ufumbuzi.

Meneja Utafiti wa TRA, Saada Ally ndiye ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 27, 2023 katika kongamano hilo ambapo amesema kupitia kongamano hilo watatambua changamoto za kurasimisha biashara, usajili na kulipa kodi zinazowakabili wafanyabiashara.

Amesema milango yao iko wazi ndiyo maana wameweka vituo mikoani ili wafanyabiashara wenye sifa waende kujisajili tayari na kuanza kulipa kodi.

Ally amesema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia  54.5 ya Watanzania wote ni walipakodi wakiwemo wafanyabiashara lakini anawahimiza wajisajili zaidi ili walipe kodi na kuchangia maendeleo ya Taifa.

"Ndio maana kila mkoa tuna vituo vya usajili ambavyo mfanyabiashara mwenye sifa anaweza akaenda akasajiliwa kwa ajili ya kuanza kulipa kodi baada ya miezi sita," amesema Ally.

Kongamano hili linaendelea katika ukumbi wa wa The Dome, uliopo Masaki jijini Dar es Salaam, limedhaminiwa na Benki ya CRDB, Kampuni ya usafirishaji ya DHL, Benki ya Stanbic, Benki ya NMB, Clouds Media, Kampuni ya matangazo ya Ashton na ukumbi wa mikutano wa The Dome.