Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA kudhibiti ubora wa bidhaa kidigitali

TRA kudhibiti ubora wa bidhaa kidigitali

Muktasari:

  • Mwananchi yeyote atalazimika kupakua App hiyo katika simu yake ya kiganjani, ikihusisha takribani nusu ya watanzania wanaotumia huduma za intaneti kama inavyoelezwa katika ripoti za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imepata mwarobaini wa kukabiliana na changamoto ya utambuzi wa bidhaa bandia baada ya kutangaza rasmi programu tumizi ya ‘Hakiki Stempu’.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, mwananchi yeyote atalazimika kupakua App hiyo katika simu yake ya kiganjani, ikihusisha takribani nusu ya watanzania wanaotumia huduma za intaneti kama inavyoelezwa katika ripoti za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata kupitia taarifa yake kwa umma aliyoitoa jana, alitoa wito huo akisema lengo ni kuhakikisha wanalinda afya za dhidi ya bidhaa bandia ikiwa ni matokeo ya uwekezaji uliofanyika katika maboresho ya mifumo ya Tehama katika mamlaka hiyo.
“Itawawezesha (App) kutambua bidhaa isiyofaa kwa matumizi na usalama wa afya zao pamoja na kuiwezesha serikali kukusanya kodi stahiki na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma nyingine za kijamii kwa manufaa ya wananchi,” ilinukuu taarifa ya kamishna huyo.
“Vile vile TRA inatoa wito kwa wazalishaji na waingizaji wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa kwa kutumia mfumo wa ETS kuwa waaminifu kwani mfumo huo una faida nyingi kwao ikiwamo kulinda bidhaa zao sokoni dhidi ya bidhaa bandia pamoja na kusaidia makadirio ya kodi kwa haki.”
 
Kuhusu matumizi ya ETS
 
Kuhusu ETS, Kidata alisema miongoni mwa maboresho ni katika stempu za kielektroniki (ETS), alama maalumu inayobandikwa au kuchapishwa katika bidhaa ili kuhalalisha bidhaa iliyozalishwa au kuingizwa nchini na mfanyabiashara anayetambulika huku akiwa amelipa kodi ya ushuru wa bidhaa stahiki.
“Kwa sasa bidhaa zinazobandikwa stempu za kielektroniki za ushuru ni bidhaa za za Sigara, mvinyo wa dhabibu, Pombe Kali, Bia, Mvinyo wa matunda mengine kama vile Ndizi, Rozela, Nyanya pamoja na aina zote za vileo,” alisema. Kidata akifafanua katika taarifa hiyo kwamba:
“Faida mojawapo ya ETS ni kulinda afya ya mtumiaji kwa kujiridhisha kuwa bidhaa hiyo imezalishwa na nani, linin a itakuwa imepita katika mikono ya vyombo vya udhibiti wa uora vya serikali na kuhakikisha kodi halali ya serikali inalipwa,” alisema.