Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TCU kufungua tena dirisha la udahili

Muktasari:

  • Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inatarajia kufungua dirisha la nne la udahili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu katika mwaka wa masomo 2019/2020 kuanzia Oktoba 1 hadi 4, 2019  ili kujaza nafasi zilizowazi katika baadhi ya program.

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) limesema litafungua dirisha la awamu ya nne ya udahili kwa wanafunzi wanaotaka kusoma vyuo vikuu nchini humo mwaka wa masomo 2019/20.

Dirisha hilo litafunguliwa kuanzia Oktoba 1 hadi 4, 2019 ili kujaza nafasi zilizo wazi katika baadhi ya vyuo ambavyo vimeomba ili kujaza baadhi ya program za masomo.

Wakati dirisha hilo likifunguliwa, waombaji waliochaguliwa katika chuo zaidi ya kimoja wameombwa kuthibitisha katika vyuo wanavyopenda kusoma hadi Septemba 30, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Septemba 25, 2019 Katibu mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema waombaji 96,338 walituma maombi katika awamu zote tatu kwa vyuo 75 vilivyoruhusiwa kudahili kwa mwaka wa masomo 2019/2020.

“Waombaji 82,758 sawa na asilimia 85.9 wamedahiliwa katika vyuo hivyo ambapo kati yao 37,450 sawa na asilimia 45 ya wadahiliwa wote walidahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja.”

“Lakini mpaka sasa waombaji 33,453 sawa na asilimia 89.3 wameshathibitisha katika chuo kimoja na wengine wanaendelea kujithibitisha na wengine wanaendelea hadi Septemba 30, 2019,” amasema Profesa Kihampa

Katibu mtendaji huyo amesema kufunguliwa kwa dirisha hilo lakini pia alivitaka vyuo vyote vya elimu ya juu kubainisha programu zilizo na nafasi ili kuwawezesha waombaji kufanya uamuzi sahihi na kuepuka usumbufu wa kuomba katika programu ambazo hazina nafasi

“Kama tume tunasisitiza vyuo vyote kuzingatia idadi ya wanafunzi iliyoidhinishwa katika programu husika na kwa waombaji wote wanakumbushwa masuala yote yanayohusiana na udahili ama kujithibitisha yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo na siyo TCU,” amesema Profesa Kihampa

“Kwa wale ambao wana changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo katika taratibu zilizowekwa,” ameongeza