Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tawa: Pori la Akiba Kilombero ni ‘Usalama wa Taifa’

amishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA ), Mabula Misungwi akizungumza kwenye semina ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, juu ya Usimamizi wa Pori la Akiba Kilombero. Lilian Lucas.

Muktasari:

  • Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma imeahidi kushiriki kwenye usimamizi wa Pori la Akiba Kilombero.

Morogoro. Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imesema Pori la Akiba Kilombero linatakiwa kuendelea kulindwa kutokana na umuhimu kwa Taifa kwani linachangia asilimia 60 hadi 65 ya maji kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere(JNHPP) linalotarajia kuzalisha Megawati 2, 115 za umeme.

Hayo yameelezwa wakati wa wasilisho kwenye semina ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, juu ya usimamizi wa pori hilo taarifa iliyotolewa na ofisi ya uhusiano ya Tawa.

Akizungumza wakati wa kutoa wasilisho hilo la Pori la Akiba Kilombero, Kamishna wa Uhifadhi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Joas Makwati amesema Pori hilo lina umuhimu kwa Taifa na kwamba umeme kutoka kwenye bwawa hilo utatumika majumbani, viwandani na kwenye shughuli za usafirishaji (reli na magari).

"Sambamba na faida hizo Pori hili ni chachu ya kufungua fursa za Utalii ikiwemo shughuli za Uwindaji wa Kitalii ambazo zinaongeza fedha za kigeni ikizingatiwa kuwa mpaka sasa Pori la Akiba Kilombero lina Vitalu vinne vya Uwindaji wa Kitalii,"amesema Makwati.

Makwati amesema katika kipindi cha Mwaka 2016/17 hadi 2020/21 Tawa ilitoa zaidi ya Sh425 milioni   kwa halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi kama gawio la asilimia 25 ya mapato yatokanayo na shughuli za Utalii katika Pori hilo la akiba.

Pamoja na faida zingine Makwati amesema Tawa imetoa fursa Kwa wananchi kufanya shughuli za uvuvi Kwa utaratibu maalumu katika pori hilo, jambo ambalo limewanufaisha wakazi wa Kilombero na Mkoa wa Morogoro kwa ujumla

Akibainisha changamoto za Pori hilo, Kamishna huyo wa kanda amesema: “Pori la Akiba Kilombero linakabiliwa na upungufu wa watumishi ambapo kwa sasa watumishi wapo 88 kati ya watumishi 279 wanaohitajika.”

Changamoto zingine zilizobainishwa ni ukosefu wa miundombinu, vikwazo katika kutekeleza kazi za halmashauri kutokana na Kijiji cha Ngombo na vitongoji 14 vya vijiji vingine kuwemo ndani ya Pori hilo pamoja na kutotekelezwa kwa sheria ya mpango wa matumizi ya ardhi ya Mwaka 2007.

Akieleza hatua za kukabiliana na changamoto hizo, amesema Tawa imeandaa mpango shirikishi wa miaka mitatu (2023 - 2025) wa usimamizi wa pori hilo ambao utakahakikisha ulinzi, uhifadhi, na matumizi endelevu ya rasilimali ya maji na Wanyamapori vinafanikiwa.

Aidha hatua nyingine zilizochukuliwa na Tawa ni pamoja na kuboresha miundombinu kwa kuweka alama za mpaka ambapo jumla ya vigingi 301 kati ya 1, 686 vimewekwa, ujenzi wa kambi mbili za doria, kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi 9, 861 wa Vijiji 16 katika Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga
Pia TAWA imeongeza vitendea kazi (gari 05, boti 04, trekta 02, na pikipiki 02), imeanzisha Kanda mbili za kiutawala Ili kuimarisha ulinzi na kurahisisha utoaji huduma Kwa wananchi na Usimamizi wa Pori.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Anderson Mutatebwa ametoa ufafanuzi wa kisera kuhusu tathmini inayofanywa na Serikali Kwa wananchi wa Kijiji Cha Ngombo na Vitongoji vilivyopendekezwa kuondolewa nje ya hifadhi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya Umma  Augustino Vuma, ameelezea juu ya kueleweka kwa wasilisho hilo na kwamba wataonyesha ushirikiano na taasisi hiyo na hivyo kulinda rasilimali za taifa.