Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania kukipaisha Kiswahili nchini Nigeria

Mkurugenzi mkuu wa TBC, Ayub Chacha (kushoto) akiwa na Mkurugenzi mkuu wa shirika la habari kutoka Nigeria Jibrin Baba wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Mashirika hayo yamesaini makubaliano ya kufanya Kazi pamoja ikiwa ni mwendelezo mzuri wa uhusiano wao tangu enzi ya ukoloni.

Dar es Salaam. Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja na Shirika la Habari kutoka Nigeria (VON) ikiwa ni mwendelezo wa uhusiano mzuri na Mashirika na Taasisi mbalimbali za Habari na Utangazaji katika Bara la Afrika.

Makubaliano hayo yamesainiwa kati ya Mkurugenzi mkuu wa TBC, Ayub Rioba na mkurugenzi mkuu wa VON Jibrin Baba Ndace ambapo yatasaidia kukuza ajenda ya Afrika kutokana na umuhimu ulionekana kwa Waafrika wenyewe kuelezea masuala yanayowahusu kwa mtazamo wa Afrika.

Mojawapo ya mashirika hayo ni Sauti ya Nigeria (VON), ambapo leo Julai 12, 2024 wamesaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja ambayo Uhusiano huo utawezesha mashirika hayo mawili kushirikiana katika masuala ya habari. 

Akizungumza makubaliano hayo, Dk Rioba amesema yanahusu kubadilishana utaalamu katika sekta ya habari na utangazaji lakini pia kubadilisha maudhui ya vipindi na matangazo mbalimbali.  

“Lengo kuu ya mahusiano hayo ni kukuza lugha ya Kiswahili kwa (TBC) kuisaidia idhaa ya Kiswahili ya (VON) kupatata watangazaji wa Kiswahili, watalaamu wa kufundisha Kiswahili na kutoa mafunzo mengine ya lugha hii,” amesema.

Mbali na hapo watashirikiana katika kubadilishana wafanya kazi katika nyanja za habari, utangazaji, ufundi wa mitambo na hadi kufika sasa tayari (TBC) imepeleka mtangazaji wake mmoja (VON) ili kusaidia katika matangazo ya Kiswahili.

Lakini pia watashirikiana katika kutoa fursa za kuwezesha kupata au kuweka wawakilishi wa vyombo vya habari katika nchi husika. Yaani (TBC) itakua na mwakilishi Nigeria na (VON) itakua na mwakilishi wake Tanzania.

Katika kuhakikisha kunakua na uhusiano wa kudumu kati ya Tanzania na Nigeria darasa la lugha ya Kiswahili limeanzishwa nchini Nigeria ili wawekezaji wa nchi hiyo waweze kutumia lugha ya Kiswahili wanapotembelea Afrika Mashariki.

Huku ikiwa kumekua na mazungumzo ya kushirikiana mafunzo ya lugha ya Kiswahili na chuo kikuu cha Port Harcourt kilichopo Nigeria.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa (VON) Jibrin Baba, amesema makubaliano yanayosainiwa leo yanaimarisha yaliyokuwepo ya historia ndefu toka enzi za Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), na Nigeria Broadcasting Corporation (NBC)

“RTD kupitia idhaa ya kingereza (external service) ilikuwa na ushirikiano wa karibu na lililokua Shirika la Utangazaji la Nigeria Nigeria Broadcasting Corporation (NBC), kwa pamoja zilihanikiza shughuli za ukombozi wa bara la Afrika”. Amesema

Hata vivyo baada ya Bara zima kupata uhuru ushirikiano huu ulififia kutakana na mabadiliko yaliotokea katika mfumo wa kisiasa na kiuchumi duniani kudhofisha umajumui wa Afrika na nchi husika kuanza utegemezi katika nyanja mbalimbali kutoka mataifa ya nje hususani Ulaya na Marekani.