Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanroads yaanza ukarabati kalavati lililotitia mto Mbwemkuru

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Baada ya kalavati lililopo katika Mto Mbwemkuru kutitia tangu Aprili 3, 2024, Wakala wa Barabara Mkoa wa Lindi, (Tanroads) wameanza kutengeneza barabara mbadala ili magari yaendelee kupita.

Lindi. Wakala wa Barabara (Tanroads) wameanza ujenzi wa barabara mbadala, baada ya kuharibika kwa kalavati katika Mto Mbwemkuru mkoani hapa tangu Aprili 3, 2024 na kusababisha magari kushindwa kupita katika eneo.

Akizungumza na Mwananchi Digital jana Ijumaa Aprili 5, 2024, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Lindi, Emily Zengo amesema kuwa maji yanayojaa kwenye mto huo yanatokana na mvua  zinazoendelea kunyesha mkoani humo na ndiyo yamesababisha kuharibika kwa kalavati hilo upande mmoja, na kusababisha magari kupita kwa zamu na kuleta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Zengo amesema kuwa barabara inayopita kwenye mto Mbwemkuru inaunganisha Wilaya ya Lindi na Kilwa na ni ya kiuchumi.

"Hata barabara ya Somanga maji yamejaa kwenye na kusababisha magari kupita moja moja, lakini kwa sasa yanapita vizuri kutokana na jitihada ambazo sisi kama Tanroad tumezifanya," amesema Mhandisi Zengo.

Upande wa barabara unaotitia kutokana na mto kujaa maji na kusababisha kutumika kwa upande mmoja wa barabara. Picha na Bahati Mwatesa

Akizungumzia kadhia hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ametoa wito kwa wenye magari kupita moja moja na wenye malori kusubiri kwa muda hadi barabara ya pili itakapokuwa tayari.

 "Kwanza niwashukuru Tanroads kwa juhudi wanazofanya za kuweka kambi hapa Mto Mbwemkuru na hadi sasa wameona bora kutengeneza barabara nyingine ili magari yaweze kupita, huku wakiendelea kutengeneza kalavati lililoharibika.”

“Niwaombe madereva wa magari ya mizigo kuanzia tani 30 kusubiri kwa muda kwani kupita upande mmoja hatari," amesema DC Ndemanga.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack ameishukuru Tanroads kwa juhudi wanazofanya kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanarejea ikiwamo kuifungua barabara  ya Somanga iliyokuwa imefungwa.

"Niwapongeze Tanroads kwa kazi kubwa wanayofanya na kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanarejea, Somanga asubuhi maji yalijaa kwenye barabara magari yalikuwa hayapiti, lakini Tanroad wamejitahidi magari yameanza kupita, niwaombe wananchi kuwa wavumilivu wakati wataalamu wetu wanajitahidi kurudisha mawasiliano ya barabara kama awali," amesema Telack.

Mkazi wa Mbwemkuru, Omary Salum amesema, "sisi wakazi wa mto Mbwemkuru tunaishukuru Serikali kwa juhudi kubwa wanayofanya ya kurudisha mawasiliano ya barabara.”