Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tamisemi yatoa msimamo kuligawa Jiji la Dodoma, yakubali hoja ya Musukuma

Muktasari:

  • Katika hoja yake, Musukuma ambayo iliungwa mkono na wabunge wengi, alilalamikia ujenzi wa maghorofa akisema si rahisi mtu kupanda juu kwa ajili ya kwenda kununua kifungo cha koti na akaenda mbali zaidi akiomba Serikali ijifunze kwa Soko la Machinga la Dodoma.

Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema hoja ya kuligawa Jiji la Dodoma katika halmashauri tatu ni ngumu kwa sasa kutekelezwa kwani itakwenda kuongeza gharama za uendeshaji.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumatatu, Juni 22, 2026 na Waziri wa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe wakati akichangia Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2026/27.

Amesema kazi itakayofanyika kwa wakati huu ni kuimarisha uongozi kwenye jiji hilo ambalo ni makao makuu ya nchi.

Waziri huyo pia amekubaliana na hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Musukuma, ambaye alilalamikia ujenzi wa masoko ya wafanyabiashara ndogondogo (machinga), akisema kwamba yanapojengwa kwa mtindo wa maghorofa yanakosa tija.

Katika hoja yake, Musukuma ambayo iliungwa mkono na wabunge wengi, alilalamikia ujenzi wa maghorofa akisema si rahisi mtu kupanda juu kwa ajili ya kwenda kununua kifungo cha koti na akaenda mbali zaidi akiomba Serikali ijifunze kwa Soko la Machinga la Dodoma ambalo lilijengwa na kujaza wafanyabiashara kwa wakati mmoja.

“Tunakubaliana na hoja za wabunge kwamba ujenzi wa masoko lazima uzingatie hali halisi ya maeneo na mahitaji kwa uhalisia, tunakwenda kufanya hivyo,” amesema Profesa Shemdoe.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amesema Serikali imekubali kuweka mifumo inayosomana kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Tamisemi ili kupunguza mivutano ya kikodi inayotokea mara kwa mara.

Kwa upande wa mikopo ya vijana, wanawake na wenye ulemavu, amesisitiza kuwa wataendelea kuitoa kwa asilimia 10 huku akieleza kuwa Serikali imekubali kurudisha asilimia 15 ya makusanyo kwa halmashauri, ambapo asilimia tano zitatumika kwa ajili ya maendeleo ili kuchochea ajira kwa vijana.