Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dodoma yatengewa fedha zaidi za barabara, Simbachawene atoa sababu

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiwasilisha bajeti ya mwaka 2026/27 leo Jumatano, Mei 20, 2026 bungeni jijini Dodoma  

Muktasari:

  • Katika miradi hiyo, mbali na barabara ya mzunguko yenye urefu wa zaidi ya kilomita 100, lakini upo upanuzi wa barabara ya Dodoma – Morogoro (kilomita 70), sehemu ya mzunguko wa Kimbinyiko hadi njia panda ya Chamwino (kilomita 32) ambayo itakuwa njia sita.

Dodoma. Wizara ya Ujenzi imeitaja miradi ya upanuzi wa barabara za majiji na manispaa kwa ajili ya kupunguza msongamano ambapo Mkoa wa Dodoma umekuwa kinara kwa kuwa na barabara nyingi kuliko maeneo mengine.

Katika miradi hiyo, mbali na barabara ya mzunguko yenye urefu wa zaidi ya kilomita 100, lakini upo upanuzi wa barabara ya Dodoma – Morogoro (kilomita 70), sehemu ya mzunguko wa Kimbinyiko hadi njia panda ya Chamwino (kilomita 32) ambayo itakuwa njia sita.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiwasilisha bajeti ya mwaka 2026/27 leo Jumatano, Mei 20, 2026 bungeni jijini Dodoma.

Hata hivyo, Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene ametaja sababu kwa nini Dodoma inaonekana kupendelewa, “kwa sababu ni mkoa unaobeba makao makuu na sura ya Taifa.”

Simbachawene pia amewavunja mbavu wabunge akisema ‘ukatikati unafurahisha lakini ukiwa katikati unakuwa salama’ hivyo wakazi wa Dodoma kuwa katikati kunawabeba na kufurahisha.

Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma ukiendelea

Kwenye taarifa ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aliyoiwasilisha leo Jumatano, Mei 20, 2026 bungeni jijini Dodoma inaonyesha bajeti ya mwaka 2026/27, barabara zinazopanuliwa ni kila upande kutoka katikati ya Jiji kwenda Iringa (kusini), Arusha (Kaskazini), Singida (Magharibi) na hiyo ya upande wa Mashariki inayokwenda Morogoro.

Ujenzi wa barabara za mzunguko Dodoma ukiendelea.

Mikoa mingine iliyopewa nafasi ya upanuzi wa barabara za miji yao ni Arusha kwa barabara ya Arusha – Kisongo (kilomita 9.3) inayopanuliwa kuwa njia nne, barabara ya Mbauda – Losinyai (kilomita 70) na Tengeru – USA River (kilomita 11.3).

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiwasilisha bajeti ya mwaka 2026/27 leo Jumatano, Mei 20, 2026 bungeni jijini Dodoma.

“Jiji la Mwanza mradi wa upanuzi kutoka njia mbili hadi nne kwa barabara ya Mwanza – Usagara (kilomita 25), barabara ya Mwanza Airport – Kayenze (kilomita 10) wakati mikoa mingine ni Mbeya, Miji ya Iringa, Songwe na Singida,” amesema Ulega.