Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taarifa kuhusu moto uliozuka Mwananchi

Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wa Kampuni ya ulinzi ya SGA wakiwa katika harakati za kuudhibiti moto uliozuka kwenye stoo zilizopo jengo la uchapaji wa magazeti MCL.

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa mashuhuda, moto huo ulioanza majira ya saa 1:30 jioni na ulidhibitiwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Zimamoto na magari ya kampuni ya SGA.

Dar es Salaam. Moto ambao chanzo chake hakijajulikana umezuka katika stoo zilizopo jengo la uchapaji wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Tabata Relini Dar es Salaam kabla ya kudhibitiwa leo Jumanne Agosti 29, 2023.

 Kwa taarifa za awali kwa mujibu wa mashuhuda zinaonesha moto huo ulianza majira ya saa 1:30 na unaendelea kudhibitiwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Kampuni ya ulinzi ya SGA.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu imesema chanzo cha moto bado kinachunguzwa.

“Chanzo cha moto huo hakijulikani wakati huu. Kipaumbele chetu kwa sasa ni usalama wa wafanyakazi wetu na kuilinda jamii inayotuzunguka. MCL inadhamiria kuendelea kuhakikisha usalama na ustawi wa watu wake. Uchunguzi unaendelea, na tutaweletea taarifa zaidi pindi utakapokamilika,” amesema Machumu.

Amesema biashara ya kampuni inaendelea kushamiri ikiwezeshwa na wasomaji wetu na wateja wetu mbalimbali.

“Tumejizatiti kuendelea kuwahudumia kikamilifu kwa kutoa habari sahihi zinazowezesha taifa na kwa kuendelea kuwapa huduma stahiki na za haraka wateja wetu wa uchapishaji na usafirishaji vifurushi,” amesema.

Ameongeza hatua za haraka kuhakikisha wasomaji hawakosi magazeti mitaani, uchapishaji unaendelea bila kukwama na kwa wale wanaotumia Mwananchi Courier, mizigo yao inasafirishwa bila usumbufu.

Maofisa wa Kampuni ya ulinzi ya SGA wakiimarisha ulinzi katika lango kuu la Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Tabata Relini Dar es Salaam.

“Kwa wale wanaotumia majukwaa yetu ya kidigitali, endelea kuwa nasi kwa habari za uhakika na uandishi mahiri. Tovuti zetu, mitandao ya kijamii, na aplikesheni zetu za Nation ePaper na eGazeti zipo tayari kuwahudumia.

“MCL inatoa shukrani za dhati kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, SGA Security na Jeshi la Polisi kwa kusaidia kudhibiti moto huo na kuhakisha usalama wa wafanyakazi wake na wa jamii inayotuzunguka,” amesema.