Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sungusia, Heche wazungumzia changamoto za teknolojia kwa mawakili

Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Vijana Nchini (TYL) Edward Heche akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa shindano la wanafunzi wa Sheria namna ya kuendesha kesi (moot court), mwaka 2023, lililoandaliwa na kampuni ya Victors Hub, jijini Dar es Salaam

Dar es Salaam. Viongozi wa mawakili nchini, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Harold Sungusia na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Vijana (TYL), Edward Heche wamewataka mawakili kutafuta maarifa mapya ili kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia na changamoto zake.

Sungusia na Heche walizungumzia changamoto hizo wakati wa ufunguzi wa fainali za shindano la uendeshaji kesi (mahakama ya mfano – Moot Court), jana katika ukumbi wa jengo la TLS  (Wakili House) jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo limeandaliwa na kampuni ya Victors Hub Limited (VICON) kwa kushirikiana na kampuni ya uwakili ya Victory Attoneys & Consultant, likiwa ni msimu wa tatu tangu mwaka 2021.

Shindano hilo linalowashirikisha wanafunzi 20, kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini waliofuzu hatua ya kwanza ya kuwasilisha hoja kwa maandishi, kwa mwaka huu lina mada inayohusu teknolojia katika masuala ya kifedha na uchumi wa kidigitali (Fintech and digital economy)

Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa shindano hilo wakili Heche alisema kuwa kwa sasa wanashuhudia mabadiliko ya haraka katika ulimwengu wa teknolojia ya kifedha na kwamba hivyo  suala la udhibiti ni muhimu sana kwa wanasheria na wanafunzi wa sheria.

“Tunapochunguza masuala haya, nawaasa kuwa na ujasiri wa kufuata maarifa na ujuzi mpya, kwani ndivyo tutakavyoweza kuelewa na kushughulikia changamoto za kisheria zinazoendana na maendeleo haya, ili  kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu”, alisema Heche.

Alisema kuwa shindano hilo ni fursa nzuri ya kuonyesha ujuzi wao wa kisheria na jinsi wanavyoweza kutumia sheria kama chombo cha kutatua changamoto za kisasa na kwamba kila changamoto ni fursa mpya ya kujifunza na kukua.

Hivyo aliwataka kuwa wabunifu, weledi, na kuzingatia maadili i na kuwataka wafanye kazi kwa bidii akisema kuwa kila hatua wanayoichukua katika shindano hilo inachangia kujenga mustakabali wao.

Kwa upande wake Sungusia aliwataka wanasheria kutokujifungia katika wigo wa tasnia hiyo pekee bali watazame fursa nyingine zinazotokana na maendeleo na mabadiliko ya kiteknolojia pamoja na kukabiliana na changamoto zake.

Alisema kuwa mwanasheria hawezi kuwa mjuvi wa sheria mbalimbali bila kujipanua zaidi nje ya eneo lake na kwmaba teknolojia inawalekeza hivyo kwa kuwa inazidi kupanuka na kuja na changamoto nyingi.

“Wengi tumekua tukijifungia ndani tunashindwa kuangalia fursa kubwa ambazo zinajitokeza baada ya Teknolojia kuongezeka. Kuna mambo mengi yanatokea sasa ambayo tunapaswa kuyazingatia yakiwemo matumizi ya akili bandia. Hivyo hata sisi wanasheria tunapaswa kutumia fursa zinazopatikana katika maendeleo ya kiteknolojia”,alisema Sungusia.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Victors Hub, waandaaji wa shindano hilo wakili Rayson Luke alisema kuwa lengo la shindano hilo ni kuwajengea vijana uwezo wa namna ya kuendesha mashauri mahakamani na kuwawezesha kuona fursa nyingine.

“Unajua kule vyuoni wanasoma sheria za kawaida tu kama vile jinai, madai, mikataba na nyinginezo lakini sasa inapokuja vitu kama hivi fintech (mifumo ya kiteknolojia ya kifedha) uchumi wa kidigitali na akili bandia wanaona kuna maeneo mapya ambayo wanaweza kuyafanyia kazi”, alisema Luka na kuongeza:

“Hii inawafanya wajue kwamba dunia inabadilika, sheria pia zinabadilika na kuna maeneo mapya ya sheria ambayo yana upungufu wa wataalamu na baada ya kumaliza vyuo wanaweza wakajikita kwenye maeneo hayo.

Luka alisema kuwa washindi katika shindano hilo watapewa zawadi mbalimbali kama tuzo, zawadi, ufadhili wa masomo ya katika Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania –LST), nafasi ya kufanya mazoezi katika kampuni za kisheria baada ya kumaliza vyuo.

Ametoa wito kwa vyuo vikuu nchi kuwa na mfumo wa mahakama hizo za mfano kama ilivyo katika nchini nyingine kwa kuwa sheria ni vitendo badala ya nadharia pekee.