Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sita wanaswa Morogoro wakidaiwa wahamiaji haramu

Muktasari:

  • Watuhumiwa hao wanaotajwa kuwa raia wa Ethiopia walikamatwa Julai 20, 2024 katika eneo la Pori la Kisisi lililopo katika Kijiji cha Malolo wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro.

Morogoro. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama limewakamata raia sita wa Ethiopia wanaotuhumiwa kuingia nchini bila kibali katika operesheni ya kukamata wahalifu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 22, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema watuhumiwa hao walikamatwa Julai 20, 2024 katika eneo la Pori la Kisisi lililopo katika Kijiji cha Malolo, Kata ya Malolo B wilayani Kilosa.

"Tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa haramu Julai 20, mwaka huu, saa tatu asubuhi, wakiwa katika eneo la Kisisi. Kule kuna pori kwa hiyo walikuwa wamejificha katika Kijiji cha Malolo, Kata ya Malolo B, Wilaya ya kipolisi ya Luhembe na tayari tumewakabidhi kwa Uhamiji washughulike nao,” amesema.  

Kwa upande wake, Naibu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro, Mrakibu Richard Mwasongwe amesema kwa kushirikiana na polisi wamewakamata wahamiaji hao wakiwa njiani kusafirishwa kuelekea nje ya nchi.

Mwasongwe, amewataka wananchi kuepuka kujihusisha na masuala ya uhamiaji harumu, kwani wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria pamoja na kutozwa faini ya Sh20 milioni. Pia kutaifishiwa mali zilizotumika kuhifadhi au kusafirishia.

"Nitoe wito kwa wananchi wote kuepuka kujihusisha na usafirishaji wa uhamiaji haramu, kwani Sheria ya Uhamiaji ya mwaka 2016, Sura ya 54 Kifungu cha 46(1)© na (2), mtu yoyote atakayebainika kufanya hivyo adhabu yake ni faini ya Sh20 millioni au kifungo cha miaka 20 jela na atakayekutwa amewahifadhi au ametumia chombo cha usafiri tutakitaifisha," amesema Mwasongwe.

Mbali na wahamiaji hao, Kamanda Mkama amesema wamefanya misako na operesheni mbalimbali, ikiwemo wizi wa mali pamoja na utapeli, ambapo wamewakamata watu watatu wanaotuhumiwa kujihusisha na uuzaji wa viwanja visivyo vyao.

Kamanda Mkama amesema watuhumiwa hao walikamatwa Julai 17, 2024 wakituhumiwa kuwauzia wananchi viwanja vya makazi vilivyopo katika maeneo ya watu wengine. Wanatuhumiwa kujipatia Sh40 milioni.

"Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa wanaandaa mikataba ya uongo, ili kuendelea kuuza viwanja katika eneo la Mkundi na sasa wamefanikiwa kuwauzia watu wengi na kujipatia Sh40 millioni kwa udanganyifu," amesema Mkama.