Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sita kizimbani wakidaiwa kumuua Milembe wa GGM

Muktasari:

  • Milembe Seleman (43) aliyekuwa mfanyakazi wa kitengo cha Ugavi katika kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu (GGML) aliuawa Aprili 26, 2023 kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani, usoni na mikononi ambapo kiganja kimoja cha mkono kiliondolewa.

Geita. Watu sita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita wakishtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya madini ya dhahabu (GGM) Milembe Seleman (43).

Watuhumiwa waliopandishwa mahakamani katika kesi namba 12/2023  ni Dayfath Maunga(30), Safari Labingo(54), Genja Lubingo(30), Musa Lubingo (33), Maige Fundikira (37) na Ceslia Macheni (55).

Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Johari Kijuwile, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Scolla Teffe ameieleza Mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa la mauji kinyume na kifungu cha 196 & 197 cha kanuni ya adhabu .

Amedai Aprili 26, 2023  Dayfath Maunga na wenzake watano huko katika maeneo ya Mwatulole wakishirikiana kwa pamoja walimuua Milembe Seleman.

Washtakiwa hao hawakupaswa kuzungumza chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 7, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wote wamerudishwa mahabusu.