Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sintofahamu wimbi la ubakaji unaofanana Singida

Muktasari:

  • Baadhi ya wanawake mjini Singida wamesimulia matukio ya ubakaji yanayofanana, huku Jeshi la Polisi mkoani likisema linamshikilia mtu mmoja anayetuhumiwa kuhusika.

Singida. Baadhi ya wanawake mjini Singida wamesimulia matukio ya ubakaji yanayofanana, huku Jeshi la Polisi mkoani likisema linamshikilia mtu mmoja anayetuhumiwa kuhusika.

 Tukio hilo ni mfululizo wa matukio ya ubakaji yanayodaiwa kutokea kati ya Novemba 7 hadi 16 mwaka huu katika mitaa ya Sabasaba na Ungakae wilayani Singida.

Miongoni mwa waathiriwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Chief Senge wilayani Singida aliyesema, aliobakwa wakati akienda dukani kumnunulia mama yake maji ya kunywa.

Akisimulia kuhusu tukio hilo jana Novemba 24, mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) amesema Septemba 7, 2023, saa 1.30 usiku akiwa njiani kuelekea dukani alikutana na kijana aliyemuomba amuelekeze njia ya kwenda Chuo cha Utumishi.

Amesema wakati akimuelekeza kijana huyo alimkaba shingoni hali iliyosababisha kupoteza fahamu na kumpeleka katika jumba ambalo ujenzi wake haujaisha (pagale).

“Nilitumwa na mama kununua maji, nikakutana na kijana aliyekuwa anaongea na simu. Alinifuata akaniomba niemuelekeze Chuo cha Utumishi. Lakini wakati namuelekeza akanikaba, nikapoteza fahamu akanipeleka kwenye pagale, nilipozinduka nikakuta anamenibaka,” amesema.

Mama mzazi wa binti huyo, (jina lake limehifadhiwa), amesema hali ya binti huyo kwa sasa sio nzuri licha ya kupatiwa matibabu.

Amesema tangu kutokea kwa tukio hilo amekuwa mtu mwenye woga kwa kila anayemuona mbele yake na hata kutoka nje amekuwa mwoga na mwenye aibu.

Kwa upande wake, msichana mwingine (23), amesema Novemba 16 akiwa katika Mtaa wa Uwanja wa Ndege alikutana na kijana aliyemuomba amuelekeze njia ya kuelekea Chuo cha Utumishi lakini wakati akifanya hivyo alimbaka na kumuamrisha amfuate anakotaka aende.

“Akaniambia nimfute, akanipeleka nyuma ya tenki la maji, akaniambia nipige magoti nikawa nakataa, nikikataa anazidi kunikaba ikanibidi tu niwe mpole nifanye anavyotaka ndipo alipofanikiwa kunibaka,” amesema msichana huyo.

Mbali na wawili hao kubakwa, binti mwingine alinusurika kubakwa katika eneo hilo baada ya baada ya kufanikiwa kupambana na kumtoroka mbakaji huyo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba, Mahmood Nkungu amesema ongezeko kubwa la watu kwenye mtaa huo linalosababisha na idadi kubwa ya wanafunzi katika vyuo vya Uhasibu na Utumishi, kumesababisha kuibuka kwa uhalifu.

Nkungu ameliomba Jeshi la Polisi kuwapatia msaada wa ulinzi kwenye eneo hilo ili kuimarisha hali ya usalama na kukomesha matukio ya uhalifu yanayosababisha uvunjifu wa amani.

Amesema ingawa yupo polisi kata mmoja, lakini anashindwa kumudu kutokana na ongezeko la watu kwenye mtaa wake.

Mmoja wa wakazi wa mtaa huo, Seif Hamis ameliomba Jeshi la Polisi kuongeza doria katika mitaa yao ili kuyabaini watu wanaofanya vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vingi katika siku za karibuni.

“Jeshi la Polisi liongeze umakini juu ya doria yao katika mitaa yetu kwa sababu matukio kwasababu wao watakuwa wananafasi zaidi kuchunguza na kuwabaini wanaofanya matukio ya namna hii,” amesema Seif

Akizungumza jana Ijumaa Novemba 24, 2023 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa amesema katika msako uliofanyika Novemba 23 mwaka huu, walifanikiwa kumkamata Mkazi wa Unyakae katika Kata ya Mandewa wilayani Singida, Innocent Vincent (24), akituhumiwa kwa makosa ya ubakaji.

Kamanda Stella amesema mtuhumiwa huyo amedaiwa kuhusika na tukio la ubakaji Januari 24, 2023 saa 2.00 usiku kwa mama mwenye umri wa miaka 31 nyumbani kwake maeneo ya Unyankae na kisha kutoroka kusikojulikana.

“Mtu huyu alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu, akituhumiwa kwa makosa ya ubakaji. Mara uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani,” amesema.