Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sintofahamu ‘Toto Afya' kuondolewa NHIF

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga

Muktasari:

  • Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetangaza kuwa watoto ambao awali walikuwa wakisajiliwa kupitia utaratibu wa bima ya afya ya ‘Toto Afya kadi, sasa watasajiliwa kupitia vifurushi vya bima ya afya au shule wanazosoma.

Dar es Salaam. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetangaza kuwa watoto ambao awali walikuwa wakisajiliwa kupitia utaratibu wa bima ya afya ya ‘Toto Afya kadi, sasa watasajiliwa kupitia vifurushi vya bima ya afya au shule wanazosoma.

Mabadiliko hayo yalitolewa jana Jumatatu Machi 13 mwaka huu katika taarifa ya NHIF kwa umma.

Taarifa ilieleza NHIF inafanya maboresho ya usajili na huduma kwa watoto waliokuwa wanasajiliwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya ya ‘Toto Afya Kadi’

“Hivyo katika kipindi hiki cha maboresho, wazazi wanashauriwa kusajili watoto wao kama wategemezi kupitia vifurushi vya bima ya afya au kupitia shule wanazosoma,” alisema.

Akifafanua taarifa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga alisema kama baba hana bima sasa anaruhusiwa kukata ili amjumuishe na mwanawe katika bima hiyo.

“Sasa hivi wanaruhusiwa kukata bima itakayojumuisha familia, tuna kifurushi kinaruhusu familia, kwa wale watoto ambao hawajaanza shule maana yake wapo kwenye mpango wa Serikali wa matibabu bure, hivyo hao hawatalazimika kuwa na bima lakini kwa wale walioanza shule wawe na bima,” alisema.

Mabadiliko hayo yamemuibua Isack Juma ambaye alisema japo Serikali inasema matibabu bure kwa watoto lakini utoaji wa huduma bado haujafikia kiwango hicho. “Ukiwa na bima ya afya unatibiwa hata hospitali binafsi lakini huwezi kusema mtoto chini ya miaka mitano atatibiwa katika hospitali binafsi bure. Hawajajiapanga, waangalie njia nzuri ya maboresho,’’ alisema.