Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simulizi ya mwenyekiti wa mtaa aliyeongoza kwa miaka 39

Mkazi wa Mtaa wa Bulibata uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Alkadi Bagani (74) akiapishwa kuwa mwenyekiti wa mtaa huo kwa kipindi cha miaka 39 sasa baada ya kuchaguliwa tena kwa miaka mitano ijayo.

Muktasari:

  • Mkazi wa Mtaa wa Bulibata, Kata Buhembe Manispaa ya Bukoba, Alkadi Bagani (74) ambaye amechaguliwa na wananchi mara kadhaa kwa vipindi mfululizo kuwa mwenyekiti wa mtaa huo tangu mwaka 1985.

Bukoba. Mkazi wa Mtaa wa Bulibata uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Alkadi Bagani (74) amekuwa mwenyekiti wa mtaa huo kwa kipindi cha miaka 39 sasa baada ya kuchaguliwa tena kwa miaka mitano ijayo.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Novemba 29, 2024 baada ya kula kiapo cha utii na uadilifu wa uongozi, Bagani amesema ameaminiwa na wananchi wa mtaa huo kwa sababu amekuwa akisaidia jamii na hupatikana muda wote pale wananchi wanapomuhitaji.

“Siri ya kuwa kiongozi kwa miaka 39 na kuaminiwa ni kwa sababu nimekuwa nikiwasaidia wananchi wangu kwa muda mwafaka, pale wanaponihitaji kutatua changamoto zao na nimekuwa mkweli kila wakati katika majukumu yangu,” amesema Bagani.

Amesema kuchaguliwa tena anaona ni matunda ya uongozi wake, hivyo hana wasiwasi na hali aliyonayo (ulemavu) wala uzee kumkwamisha katika kazi.


Elimu yake

Bagani alizaliwa mwaka 1950 alisoma katka Shule ya Msingi Nyakato, iliyopo Bukoba mwaka 1963, baadaye alichaguliwa kwenda Nyarugongo Middle School alikohitimu mwaka 1967, kabla shule hiyo haijbadilishwa jina kuitwa Katoma.

Amesema hakuendelea na elimu ya sekondari bali aliishia hapo kutokana na utaratibu wa kielemu miaka hiyo.

Ameishauri Serikali kuendelea kuwasaidia watu wenye na wazee kupata matibabu ya kuaminika katika vituo vya afya, zahanati na hospitali kwa kupata matibabu kamilifu.

Mkazi wa Mtaa wa Bulibata, Ashura Juma amesema ameshuhudia mzee huyo akiongoza kwa ustadi, waledi, utulivu na uadilifu kwa kuwajali wananchi wake katika kutatua migogoro, ikiwemo ya familia, hivyo wanazidi kumwamini na kumpigia kura awe kiongozi wao.

“Haijalishi hali aliyonayo, nampenda sana kwa sababu ni mchapaka kazi, ukienda na tatizo analitatua au kulisukuma mahali husika ili lipatiwe ufumbuzi, nimefurahi sana na nimemchagua mwenyewe kwa kura yangu,” amesema Ashura.