Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SIKU YA BABA DUNIANI: Kinababa wa 'Millennial' ndio kinababa bora kuwahi kutokea

Muktasari:

Lakini kinababa wa kizazi hiki hatuko hivyo; tunashiriki maisha ya watoto wetu, tunakwenda kwenye mikutano ya shule mpaka klinki, tunacheza na watoto wetu na hata kubadilisha ‘diapers’ kwetu sio tatizo.

Kwanza, kabla hatujafika mbali, millennial ni kundi la watu waliozaliwa miaka ya 1981 mpaka 1996. Kwahiyo kama kwa mwaka huu una umri wa miaka kati ya 29 hadi 41 wewe ni millennial.

Teaser: Kwanini kinababa wa kizazi hiki ni baba bora kuliko baba wote kuwahi kutokea? Ni kwa sababu tumeziba mapengo ambayo baba wa vizazi vilivyopita kama vile kizazi X na ‘Baby Bomers’ walishindwa kuyaziba.

Tangu dunia iumbwe, haijawahi kuwa na kinababa bora zaidi ya wale wa kizazi cha ‘millennial’. Huu si ushindani, ni uhalisia na nitakwambia kwa nini.

Kwanza, kabla hatujafika mbali, millennial ni kundi la watu waliozaliwa miaka ya 1981 mpaka 1996. Kwahiyo kama kwa mwaka huu una umri wa miaka kati ya 29 hadi 41 wewe ni millennial.

Kwanini kinababa wa kizazi hiki ni baba bora kuliko baba wote kuwahi kutokea? Ni kwa sababu tumeziba mapengo ambayo baba wa vizazi vilivyopita kama vile kizazi X na ‘Baby Bomers’ walishindwa kuyaziba.

Kwanza, kushiriki kwenye maisha ya watoto na familia zetu ni kipaumbele. Kinababa wa vizazi vilivyopita walikuwa wanaamini kuwa baba ni kuhudumia familia tu, lakini masuala ya kushiriki kwenye familia na maisha ya mtoto hayawahusu.

Unakuta baba analipa ada kuanzia shule ya msingi mpaka chuo na hajawahi kuhudhuria kikao cha shule wala mahafali na usikute hata jina la shule anayosoma mtoto wake haijui.

Lakini kinababa wa kizazi hiki hatuko hivyo; tunashiriki maisha ya watoto wetu, tunakwenda kwenye mikutano ya shule mpaka klinki, tunacheza na watoto wetu na hata kubadilisha ‘diapers’ kwetu sio tatizo.

Kinababa wa vizazi vilivyopita walikuwa wanaona kufanya shuhuli kama hizi ni kama kupoteza uanaume na ubaba wako.

Pili, tunakumbatia usawa wa kijinsia. Hatuna yale mambo ya sisomeshi mtoto wa kike, akikua ataoelewa. Sisi tunapeleka watoto wa kike shule kama ambavyo tunapelekea watoto wetu wa kiume.

Kwetu wote ni watoto, wote wanahitaji fursa sawa bila kujali jinsia, jambo ambalo halikuwa hivyo kwa kinababa wa vizazi vilivyopita.

Tatu, kinababa wa kizazi cha millennial tunawapa watoto wetu uhuru wa kujieleza. Mfano, majuzi nilikuwa hospitalini, nikamsikia baba wa millennial anamwambia mtoto wake wa kama miaka minne hivi akae kwenye kiti, mtoto akakataa akisema “hapana.”

Mzee mmoja, baba wa vizazi vilivyopita akaninong’oneza, “watoto wa siku wanalelewaje”. Kwake yeye mtoto kusema hapana kwa baba yake ni jeuri, ni kukosa adabu.

Lakini kwa yule baba wa kizazi hiki haikuwa hivyo, alianza kumuuliza mwanawe kwanini hataki kukaa, alimpa uhuru wa kujielezea, ili pengine akimuelewa anaweza kuwa msaada kwa changamoto anayopitia.

Kweli, mtoto akawa anaonyeshea ‘uchafu’ kwenye kiti, kumbe kulikuwa na juisi iliyomwagika.

Nne, tunajali afya za akili. Habari za kusema wewe ni mtoto wa kiume, hutakiwi kulia, pambana, hatutaki kuzisikia.

Kupambana tunapambana kama kawaida kwa sababu ni kweli mwanaume lazima upambane, lakini na kulia pia tunalia kwa sababu inatusaidia kushusha mzigo wa msongo wa mawazo ambao mwanaume anaukabili. Kinababa wa kizazi hiki hatuoni aibu kuomba msaada kwa wake zetu pale mambo yanapokuwa magumu kwa kuhofia wataudharau uanaume wetu.

Hatuoni haya kuomba msamaha kwa watoto na wake zetu pale tunapokesea kwa kuhofia watatuona sio marijali. Hakuna mtu aliyepoteza urijali wake wake kwa kusema samahani mke wangu au hapa nimefika ukomo mke wangu naomba msaada wa mawazo.

Narudia tena, hayakuwa mashindano kati ya vizazi vilivyopita na kizazi hiki, ilikuwa ni kueleza uhalisia. Lakini pia naamini kinababa wa vizazi vilivyopita wamechangia kwa kiasi kikubwa kinababa wa millennial kuwa hivi tulivyo,  kwa sababu sisi tumelelewa na wao kwa hiyo hongera kwa wote.

Nawatakia kinababa wote,  heri ya Siku ya Baba Duniani.