Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheria vyama vya ushirika ziangaliwe

Viongozi wa chama cha ushirika cha MSN Saccoss.

Muktasari:

  • Waomba maboresho kwenye sheria za ushirika wa akiba na mikopo,elimu yahitajika kwenye masuala ya fedha kwa wawekaji fedha za Saccos.

Dar es Salaam. Serikali imeombwa kupitia upya sheria za vyama vya ushirika vya akiba na mikopo katika ukopaji wa mara tatu ya fedha zilizowekwa.

Akizungumza katika mkutano wa pili wa MSN Saccoss uliofanyika leo Jumapili Novemba 5,2023 jijini Dar es Salaam, Wakili Mwandamizi mahakama Kuu  Mussa Mwapongo amesema kuna haja Serikali kufanyia marekebisho ya sheria inayomtaka mtu kupewa mkopo mara tatu ya fedha zake pia kubadilisha vigezo vya elimu kwa wajumbe wa bodi.

Amesema sheria wakati zinatungwa zililenga wafanyakazi ambao wanategemea mishahara,tofauti na sasa kumekuwa na kada tofauti.

"Siku hizi wanajiunga watu tofauti wakiwepo wafanyabiashara kuwepo kwa sharti la elimu kwa wajumbe linawanyima fursa wenye uwezo wa kusimamia shughuli za ushirika wakati wabunge wanatakiwa kujua kusoma na kuandika na wanatoa maamuzi mengi ya nchi,"amesema Mwapongo.

Amesema kuna watu wanauzoefu wa kuendesha shughuli za biashara hivyo ni rahisi kusimamia shughuli za ushirika wao tofauti na kuwepo kwa mtu mwenye elimu lakini hana uzoefu.

Pia Mwapongo amesema kipengele cha ukopoji wa maratatu ya pesa walizojiwekea wanaushirika inawanyima uhuru wafanyabiashara kukopa mikopo mikubwa ili kuendeleza biashara zao.

Kwa upande wake Ofisa ushirika akizungumza kwa niaba ya Mrajisi msaidizi mkoa wa Dar es Salaam, Valentina Shija amesema washirika wanatakiwa kupata elimu kuhusu masuala ya fedha ili kuwasidia katika uwekaji na ukopaji kwenye Saccos zao.

"Kukiwa na elimu hakutakuwa na urasimu wa mikopo kwa viongozi kutoa mikopo kwa njia isiyosahihi, mwanzo wa mkopo mbaya ni viongozi kukubali kutoa mikopo bila mpangilio," amesema Shija.

Amesema vyama vingi vimeanguka kutokana utolewaji mbovu wa mikopo kwa kutofuata utaratibu uliowekwa na ushirika na kukosekana kwa elimu inayohusu masuala ya fedha.

“kila jambo linahitaji elimu hivyo kuna haja ya kushiriki semina zinazoandaliwa ili kuweza kujifunza na endapo mtaendelea kujifungia hamtojua Dunia inaendaje katika masuala ya fedha na itakuwa ngumu kusonga mbele,”amesema.

Awali Mwenyekiti wa Ushirika wa Mbeya,Songwe,Njombe (MSN Saccos) Michael Muywanga amesema mitaji midogo imesababisha ukosefu wa mikopo kwa kipindi cha mauzo ya juu hivyo inakuwa ngumu kuhudumia wanachama wao kwa viwango wanavyovihitaji.

Amesema mwaka 2022 walikusanya mapato ya Sh 133milioni na  mwaka 2023 wamekusanya Sh 592 milioni huku wakitoa Sh 1 bilioni kwa ajili ya mikopo kwa wanachama wao 50.

"Wafanyabiashara wanahitaji mikopo mikubwa mtu anahitaji Sh 100 milioni ukimwambia akope mara tatu ya hisa zake ni ngumu ukiangalia ameweka Sh 25 milioni hili ni la kuangaliwa tena,"amesema.

Amesema ukopeshaji wa mara tatu ya akiba zilizowekwa imekuwa ni kikwazo kikubwa cha watu kushindwa kusonga mbele kwani kuna watu wanahitaji mikopo mikubwa.

“Tumekuwa na changamoto nyingi lakini kuna sera za ushirika zinatubana pia ukosefu wa elimu kwa wanachama kuhusu ushirika wa mikopo bado halijawafikia na hivyo kuwapa ugumu katika uwekaji wa fedha,”amesema Muywanga.