Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Hakuna usawa wa ajira kwenye vyama vya ushirika na mikopo nchini’

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk Benson Ndiege akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti uliofanyika kuhusu 'Taarifa ya Utendaji Kazi wa Saccos kwa Mwaka 2022'. Picha na Mgongo Kaitira

Muktasari:

Taarifa ya kutokuwepo uwiano huo wa shughuli na ajira katika Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (Saccos) nchini imetolewa na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk Benson Ndiege.

Mwanza. Utafiti uliofanywa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) umebaini kutokuwepo uwiano kati ya wanawake na wanaume kwenye shughuli na ajira zinazotolewa katika Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (Saccos) nchini.

Taarifa hiyo imetolewa Ijumaa Septemba 22,2023 na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk Benson Ndiege ambaye amesema ripoti ya utafiti uliofanyika kuhusu 'Taarifa ya Utendaji Kazi wa Saccos kwa Mwaka 2022' ajira 13,676 zilitolewa katika vyama hivyo.

Kati ya ajira hizo, ni asilimia 70.6 sawa na ajira 9,653  zilitolewa kwa wanaume na wanawake ni 4,023 sawa na asilimia 29.4, ikilinganishwa na wanawake 6,038 waliokuwa wameajiriwa kwenye ajira 14,976 zilizotolewa mwaka jana katika vyama hivyo.

"Tunafikiria kwa nini kwenye miongozo yetu ya uchaguzi tusiweke kipengele cha kuweka limit (ulazima) ya idadi ya wanawake kwenye bodi za vyama vyetu vya ushirika. Tunalifanyia kazi hilo," amesema Dk Ndiege, huku akidokeza kuwa vyama vinavyoongozwa na wanawake vinafanya vizuri.

Mrajis huyo amesema takwimu hizo zinatoa ishara kwamba hatua zinahitajika kuchukuliwa ili kuleta uwiano na usawa wa kijinsia katika ajira na shughuli zinazotolewa kwenye Saccos nchini ili kufikia lengo la ukombozi wa kiuchumi kwa jamii.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba amewataka wanawake kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa katika vyama hivyo huku akisisitiza bodi za vyama hivyo kuzingatia kanuni na miongozo ya uendeshaji wa vyama hivyo ikiwemo usawa wa kijinsia.

Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Barani Afrika (Accosca) na Mwenyekiti wa Saccos ya Shirika la Umeme Tanzania, Somoe Nguhwe ametaja mfumo dume kuchangia kukosekana kwa uwiano huo.

“Juhudi zinahitajika kufanyika ili kuhamasisha wanawake kujitokeza kuomba nafasi za ajira na kuomba mikopo katika vyama hivyo. Tumeshaanza kuhamasisha ndiyo maana hata mimi ni kiongozi lakini idadi haitoshi ikilinganishwa na uwiano wa idadi ya watu nchini,"amesema

Katika hatua nyingine, Dk Ndiege amesema utafiti huo umeonyesha kuna ukuaji wa vyama vya AKiba na Mikopo nchini mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo mwaka juzi Saccos 580 ndiyo zilizokuwa na leseni huku mwak huu zikiongezeka na kufikia  759 mpaka Disemba 2022.

Dk Ndiege amesema Saccos nchini zinamiliki mali zenye thamani ya Sh1.2 trilioni, huku asilimia 51.4 zikiwa zinamilikiwa na vyama 16 pekee na asilimia 9.67 ya mali zote zikiwa zinamilikwa na vyama 567.

"Hii inatuonyesha kitu kama tume (TCDC) kama wadau kufanya hivi vyama vingi ambavyo vinamiliki asilimia sita viongeze umiliki katika mali za Ushirika hali hiyo haitofautiana na umiliki katika vyama vya amana, vyama vingi bado ni vidogo vinatakiwa kulelewa," amesema Dk Ndiege