Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheikh akemea siasa za udini

Shehe wa wilaya ya Wanging'ombe Mbaraka Mpanye akizungumza wakati wa kikao maalum kilichofanyika huko wilayani wanging'ombe mkoani Njombe

Muktasari:

  • Amesema yapo baadhi ya maeneo kumekuwepo na chokochoko za kidini kitu ambacho siyo kizuri hasa katika kipindi hiki Taifa linaelekea kwenye jambo kubwa la uchaguzi utakaofanyika Oktoba  mwaka huu.

Njombe. Jamii imetakiwa kukemea siasa za udini ambazo zinatolewa na mtu au kikundi cha watu kwa malengo fulani hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, kwani bila ya kufanya hivyo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani hapa nchini.

Wito huo umetolewa leo Juni 22, 2025 na Sheikh wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mbaraka Mpanye katika kikao maalumu kilichofanyika wilayani humo.

Amesema yapo baadhi ya maeneo kumekuwepo na chokochoko za kidini kitu ambacho siyo kizuri hasa wakati huu Taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu.

Amesema siasa za kuhubiri udini kwa sasa zimepitwa na wakati hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na kuchukua tahadhari kwa kuwakataa viongozi ambao watatumia dini kama silaha ya kupata uongozi.

Amesema maendeleo ya sehemu yoyote ile hayawezi kuwepo kama hakuna umoja na upendo miongoni mwa jamii kwani ushirikiano utakosekana na hata shughuli za kiuchumi zitadorora.

Mkuu wa wilaya hiyo, Zakaria Mwansasu amesema wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali wasisite kufika ofisi kwake na kutoa taarifa yoyote ambayo wanadhani inaweza kuwa msaada kwa maendeleo ya wilaya hiyo.

"Msisite kutuambia na kutukumbusha pale ambapo utaona kuna jambo linahitaji mkuu wa wilaya , mkurugenzi au mkuu wa taasisi anahitaji kulishughulikia tuambie usije ukakaa kimya au ukatembea kinyonge" amesema Mwansasu.

Mkazi wa kijiji cha Usalule, Rogart Msemwa amesema hawapo tayari kuona wananchi wanagawanywa kwa misingi ya udini katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.