Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh1.9 bilioni kuboresha mizani ya magari Mikese, Mikumi

Muktasari:

  • Msongamano wa magari uliokuwapo katika mizani ya Mikumi na Mikese huenda ukafikia tamati baada ya Serikali kutenga Sh1.9 bilioni kwa ajili ya maboresho ya mizani hiyo na kuongeza mizani mipya.

Morogoro. Takribani Sh1.9 bilioni zinatarajiwa kutumika kufanya upanuzi na maboresho ya mizani za Mikumi na Mikese huku ujenzi huo ukitajwa kusaidia kupunguza msongamano wa magari uliokuwapo awali.

Maboresho yanayokwenda kufanyika, yataondoa ulazima wa magari yote kuingia mizani na badala yake mengine yatakuwa yakipitiliza.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mhandisi Mussa Kaswahili ambaye ni Msimamizi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi kutoka Wakala wa barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Morogoro amesema utahusisha uongezaji wa mizani mpya katika eneo la Mikumi na kufanya maboresho uliokuwapo.

Kabla ya hapo magari yote yaani yanayotokea Iringa kuelekea Morogoro na yale yaliyokuwa yaliyokea Morogoro kwenda Iringa yalikuwa yakitegemea mizani moja jambo ambalo sasa litafikia tamati.

"Katika upande wa Mikumi tutafanya uboreshaji wa mzani iliyokuwapo na kuongeza mwingine katika upande wa uelekeo wa Iringa ili kuondoa msongamano wa sasa.

Maboresho hayo pia yataondoa ulazima wa magari yote kuingia mzani kupima na sasa utawekwa mfumo ambao utakuwa ukichuja magari na yale yenye uzito wa wastani yatapitiliza moja kwa moja bila kupimwa.

"Yale ambayo yataonyeshwa kuwa yanatakiwa kuhakiki uzito yataingia kwenda kupimwa, jambo hili litaondoa msongamano uliokuwapo awali kwani magari mengi yalikuwa yakisubiri kupima katika mzani mmoja.

Amesema maboresho ya mizani hizo yameanza kufanyika Februari mwaka huu na yanatarajiwa kukamilika Juni 30 mwaka huu huku akieleza kuwa hadi Septemba mwaka huu sehemu zote zitakuwa zimeanza kutumika.

"Katika mizani ya Mikese tunaongeza mfumo wa kuondoa ulazima wa magari yote kuingia mizani katika mzani wa upande wa kuelekea Dar es Salaam,"

"Hili litaenda sambamba na ujenzi mzani ambao utakuwa na uwezo wa kupima magari kwa mitaimbo yote kwa pamoja tofauti na sasa inapopima mtaimbo mmoja mmoja na hii itaondoa kero ya msongamano wa maroli katika eneo hilo.

Kristo Ilic ambaye ni Mkandarasi kutoka kampuni ya C.G.T Controctors Limited Morogoro alisema matengenezo ya kisasa yanayofanyika yatasaidia kuongeza ufanisi.

"Tunatarajia kukamilisha kazi hii ndani ya mida tuliopewa na ikiwekezana kabla ya muda uliopangwa.

Janson Maleale ambaye ni mmoja wa madereva wa magari makubwa aliyekuwa akisubiri huduma katika mizani ya Mikumi alilianbia Mwananchi kuwa kukamilika kwa unenzi huo kutapunguza kero ya kusubiri kwa mida mrefu waliyokuwa wakikuatana nayo.

"Haya maeneo ya mizani bwana yana siku na siku, kuna siku hakuna shida kuna siku unaweza kukaa hapa hadi ukasema hiki nini, sijui huwa kinatokea nini lakini huu mfumo wa kuonda ulazima wa magari yote kuingia mizazi utasaidia sana," amesema Maleale