Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatoa kibano kwa waajiri wadaiwa sugu

Muktasari:

  • Siku moja baada ya Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kuingilia kati changamoto za mafao ya wastaafu, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ametangaza kibano kwa waajiri wenye madeni sugu.

Dodoma. Serikali imeagiza mameneja wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwasilisha majina ya waajiri sugu wanaodaiwa michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku saba kuanzia leo.

Agizo hilo limekuja siku moja baada ya Spika wa Bunge, Dk Ackson Tulia kuagiza kuchukuliwa kwa hatua kwa waajiri walioshindwa kupeleka michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii, hali ilinayosabisha kero kwa wastaafu nchini.

Akizungumza Jumanne Juni 20,2023 akiongozana na wawakilishi wa Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Katambi amewataka mameneja wa mikoa kuhakikisha kuwa hakuna malalamiko ya wanachama katika mikoa wanayoiongoza.

“Sasa hii ni kipimo kwamba badala Rais (Rais Samia Suluhu Hassan) kupokea ujumbe kutoka kwa wastaafu kumlalamikia tafsiri yake ni kuwa mstaafu hajahudumiwa ipasavyo hajapata elimu ama amepuuzwa,”amesema.

Amesema malalamiko hayo kwa viongozi pia yanatafsiri kuwa hajapewa huduma inayostahili na ndio maana wanakata rufaa kwenda ngazi za juu.

Pia Katambi ameagiza mifuko hiyo kuhakikisha kuwa inawalipa wanachama ndani ya siku 60 za kisheria wanachama ambao nyaraka zao zimewasilishwa kwa ukamilifu.

 “Mameneja wahakikishe kuwa hakuna malalamiko ya wanacham akatika mikoa wanayoiongoza na kuhakikisha kuwa waajiri wote wanalipa na kuwasilisha madeni ya michango ya watumishi wao kila mwezi,”amesema.

Mbali na hilo, Serikali imeagiza mifuko ya hifadhi ya jamii kukamilisha zoezi la kusaini mikataba ya kulipa madeni ya michango ya wanachama kabla ya Juni 30, 2023.