Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatenga Sh6 bilioni kusambaza vifaatiba

Muktasari:

  • Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Jerry Silaa amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetengewa Sh6 bilioni kati ya Sh200 bilioni zilizotengwa na serikali nchi nzima kwa ajili ya vifaa tiba kwenye vituo vya afya vilivyojengwa.

Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Jerry Silaa amesema katika Sh200 bilioni zilizotengwa  na serikali kwa ajili ya vifaa tiba kwenye  vituo vya afya  na hospitali, Halmashauri ya Jiji la Ilala imepewa Sh6 bilioni.

 Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo, Septemba 25, 2023 baada ya kuhitimisha ziara ya kukabidhi vifaatiba hivyo vyenye thamani ya Sh500 milioni kwenye vituo vitatu vya afya katika Jimbo la Ukonga.

"Vifaa tulivyokabidhi ni pamoja na vitanda vya kisasa 25, mashuka 300 na mashine ya kupumulia mama wajawazito moja katika kila kituo cha afya, tulichotembelea na hiyo ni zama ya Serikali katika kuhakikisha vituo vyote vya afya vilivyojengwa vinakuwa na mahitaji yote muhimu," amesema Silaa ambaye ni Mbunge wa Ukonga.

Alisema vifaa hivyo vinatolewa na Bohari ya Dawa (MSD) kama mfanyabiashara wa shughuli zote za vifaa tiba na vitawasaidia wagonjwa kwenye vituo kutokusumbuka kwenye mbali kutafuta huduma.

Mganga  Mfawidhi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk Zaituni Hamza amesema baada ya Serikali kujenga vituo vingi vya afya viongozi wa halmashauri tulikubaliana kununua vifaa tiba ili kukidhi matarajio.

"Tulienda kuongea na MSD wakatidhibitishia vifaa vipo na tumeanza mchakato wa kuvigawa katika vituo mbalimbali vya afya kuanza juzi tunapokea vifaa na kuvigawa na kesho tunaingia jimbo la Segerea," amesema.

Amesema vifaa wanavyotoa ni mashine moja yenye thamani ya Sh150 milioni katika kila kituo kwa ajili ya kuwasaidia wajawazito.

"Sahizi huduma ya mama na mtoto vifaa vimejaa na lengo ilikuwa kulisaidia kundi hili ambalo lilikuwa na changamoto," amesema.

"Bajeti yetu ni Sh6 bilioni lakini fedha tunazozikusanya kwenye huduma ya hospitali zetu ni asilimia 50 ambayo ni zaidi ya Sh250 milioni kila mwezi," amesema.

Awali, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Pugu Kajiungeni, Dk Meshack Charles ameshukuru kwa kuwawezesha kupata vifaa tiba, huku akieleza kupewa mashine maalumu ya kupumua itakuwa mkombozi kwa kina mama.

"Mashine hizi itatusaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto, wengi walikuwa wanafariki kwa kukosa hewa kutokana na vifaa tulivyokuwa tunatumia ni vya zamani," amesema.

Amesema kituo hicho ni kikubwa na kinahudumia wagonjwa wengi ambapo kwa siku wanahudumia wagonjwa 150 hadi 400.

Vituo vya afya alivyotembelea na kugawa vifaatiba ni pamoja na Majohe, Pugu na Zingiziwa.