Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yataja kilichokwamisha fidia Kipunguni

Muktasari:

  • Mawaziri wawili wamehitimisha hoja zao zao za Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2024/25 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2024/25 huku wakiahidi kuzingatia mawazo ya wabunge.

Dodoma. Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema kilichochelewesha malipo ya fidia kwa wakazi wa Kipunguni jijini Dar es Salaam ni kubainika kuwa baadhi ya watu walishapewa fidia maeneo mengine.

Dk Mwigulu aliyasema hayo leo Novemba 10,2023 wakati yeye na Waziri wa Uwekezaji na Mipango, Profesa Kitila Mkumbo wakihitimisha hoja yao ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2024/25.

Akizungumza Dk Mwigulu amesema kilichowachelewesha kulipa Septemba si kwamba fedha zilikosekana za kulipa fidia bali kulipofanyika uhakiki iligundulika kati yao kuna ambao walishapewa maeneo mengine lakini majina yao yalikuwepo tena katika fidia.

“Kwa hiyo ilibidi kufanyika utaratibu ili masuala ya fidia yaweze kuendelea. Tunaamini baada ya kumaliza mzozo huo ndani ya mwezi mmoja tutaenda kulipa Kipunguni na maeneo mengine ambayo yenye kesi kama hiyo,”amesema.

Aidha, Dk Mwigulu amewataka maofisa wote masuhuli nchini kufuatilia fedha za umma na kuchukua hatua, huku akisema  gharama ya utawala wa sheria ni kufuata utaratibu.

Kuhusu maeneo wananchi wanayopisha miradi ya umwagiliaji, Dk Mwigulu amesema maeneo ambayo yanafanyika miradi ya maendeleo ya umwagiliaji wananchi watakaopisha watakuwa sehemu ya miradi kwa kupewa maeneo ya kilimo katika miradi hiyo.

Naye Waziri wa Uwekezaji na Mipango, Profesa Kitila Mkumbo amesema kupitia mjadala huo wameendelea kubaini kero za wananchi ambazo wamezipokea na watazingatia.

“Tumewasikia wananchi wote wanaoishi karibu na hifadhi mbalimbali nchini kwa niaba ya Rais (Samia Suluhu Hassan) wetu na mawaziri nipende kuwaambia Rais wetu anadhamini maendeleo ya wananchi kuliko kitu chochote, kila kitu tunachokifanya ni kila mwananchi anufaike,”amesema.