Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yakabidhi Sh126 milioni kwa familia zilizopoteza ndugu zao ajalini Same

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu (wa tatu kulia aliyesimama) akitoa mkono wa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali ya magari  mawili kugongana wilayani same na kusababisha vifo vya watu 42.

Muktasari:

  • Waliofariki katika ajali hiyo ni watu 42, ambapo kwenye gari dogo aina Coaster walifariki watu 31 waliokuwa wanakwenda harusini mjini Moshi, huku kwenye basi la Chanel One wakifariki watu 11.

Moshi. Serikali imetoa zaidi ya Sh126 milioni kwa familia zilizopoteza ndugu zao katika ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro ambapo kila familia imepewa Sh3 milioni kwa ajili ya taratibu mbalimbali za maziko.

Pamoja na kupewa fedha hizo, Serikali imegharamikia majeneza pamoja na kusafirisha miili hiyo kwa ajili ya taratibu za maziko wilayani Same.

Ajali hiyo ilitokea Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same mjini ikihusisha basi Kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa likitokea Same Mjini kwenda Moshi kugongana uso kwa uso kisha kuwaka moto wakati abiria wakiwa ndani ya magari hayo.

Waliofariki katika ajali hiyo ni watu 42, ambapo kwenye gari dogo aina Coaster walifariki watu 31 waliokuwa wanakwenda harusini mjini Moshi, huku kwenye basi la Chanel One wakifariki watu 11.

Shughuli ya kuaga miili hiyo, inaendelea katika viwanja vya hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Wengine ni viongozi mbalimbali wa dini, wabunge wanaomaliza muda wao Mkoa wa Kilimanjaro, ndugu jamaa na marafiki ambao wameshiriki kwenye kuaga.

Akitoa salamu za rambirambi Mbunge wa Same Magharibi, David Mathayo amesema katika jimbo lake walifariki watu 33 kutoka kata mbalimbali za jimbo hilo.

"Ndugu waombolezaji katika jimbo langu wamefariki watu 33 kutoka katika kata mbalimbali, huu ni msiba mkubwa sana ambao umetokea katika jimbo langu,"amesema Mathayo. 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.