Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diogo Jota wa Liverpool, mdogo wake wafariki ajalini

Muktasari:

  • Jota, alijiunga na Liverpool mwaka 2020 akitokea Wolverhampton.

Zamora, Hispania. Dunia ya soka imepigwa na butwaa kufuatia kifo cha mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Ureno, Diogo Jota.

Jota na mdogo wake Andre Jota wamefariki leo Alhamisi Julai 3, 2025, kwa ajali ya gari.

Jota amefariki dunia siku 13 tu tangu afunge ndoa na mpenzi wake, Rute Cardoso. Amefariki akiwa na miaka 28 na ameacha watoto watatu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ureno, Jota alikuwa akisafiri pamoja na mdogo wake, Andre Jota, ambaye pia ni mchezaji wa mpira mwenye umri wa miaka 26. Gari lao limepata ajali katika barabara ya A-52, mkoa wa Zamora, Kaskazini Magharibi mwa Hispania.

Taarifa ya idara ya dharura ya Castilla y León nchini imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa gari lililopata ajali lilikuwa likiwaka moto.

"Chumba cha dharura cha 1-1-2 kilipokea simu kadhaa zikieleza ajali ya gari katika kilomita ya 65 ya barabara ya A-52, eneo la Cernadilla, Zamora. Gari lilikuwa linawaka moto," ilisomeka sehemu ya taarifa rasmi.

Vikosi vya zimamoto kutoka mkoa wa Zamora, polisi wa barabarani na kikosi cha huduma ya afya kutoka Mombuey Health Center walifika eneo la tukio, wamethibitisha vifo vya watu wawili papo hapo ambao ni Jota na mdogo wake.

Jota enzi za uhai wake ameisaidia Klabu yake ya Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mara mbili msimu 2019/20 na 2024/25 akiwa amecheza michezo 182 na kufunga mabao 65.

Pia ameiwezesha timu yake ya taifa ya Ureno kutwaa kombe ya Uefa Nations League akiwa amecheza mechi 49 na kufunga mabao 14.