Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaingilia kati wananchi kutoandika wosia

Serikali yaingilia kati wananchi kutoandika wosia

Muktasari:

  • Wizara ya Katiba na Sheria imeipa jukumu Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kudodosa wananchi sababu za kutoandika wosia.

Dar es Salaam. Wizara ya Katiba na Sheria imeilekeza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kukusanya maoni kwa wananchi ili kubaini sababu zinazofanya kuwa na mwitikio mdogo katika kuandika wosia.

Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo amesema ipo haja kwa Serikali kutambua kiini cha hali hiyo na kuona namna ya kutatua ili kupunguza migogoro ya mirathi ambayo kwa kiasi kikubwa waathirika ni wanawake na watoto.

Akizungumza leo wakati wa mkutano wa mamlaka hiyo na wadau Mary amesema licha ya hamasa kubwa kutolewa kuhusu umuhimu wa wosia mi watanzania wachache ambao tayari wameandika wosia.

“Tunawaelekeza Rita kuandaa dodoso ipelekwe kwa wananchi waeleze sababu zinazofanywa washindwe kuandika wosia, tumefika huku maana migogoro imekuwa mingi ambayo ingeweza kuzuilika.

“Kuandika wosia haimaanishi unajichulia, bali unaweka mazingira mazuri kwa wale utakaowaacha duniani ikitokea Mungu ametangulia kukuchukua. Hili ni suala muhimu na tunapaswa kuzingatia,” amesema Mary.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Rita, Angella Anatory amesema mamlaka hiuo imepokea wosia 700 pekee idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na takwimu za namba ya watanzania.

“Tunatambua kuwa kuna taasisi nyingine zinazohusika katika uandaaji na utunzaji wa wosia kama benki na wanasheria binafsi lakini upande wa Serikali, Rita ndio inafanya kazi hiuo niwasisitieze watanzania kuandika wosia.

“Maelekezo ya wizara tunayafanyia kazi tumeandaa dodoso ya ndani kwanza ipitiwe na menejimenti kabla ya kuipeleka kwa wananchi tupate maoni yao kwanini wanakuwa wazito kuandika wosia,” amesema Angella.