Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali: Wajasiriamali zalisheni bidhaa kukidhi soko

Mkurugenzi wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido), Shome Kibende aliyemwakilisha Waziri wa Viwanda, Ashatu Kijaji, kati kongamano la wajasiriamali wachanga, wadogo na kati (MSMEs) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la hilo

Muktasari:

  • Serikali imewataka wajasiriamali nchini kuzalisha bidhaa zinazokidhi vigezo vya ubora kwa kuangalia fursa zilizopo sokoni ili kukidhi soko la ndani ya nchi, Afrika Mashariki na nje ya bara ili kukua kibiashara.

Dar es Salaam. Serikali imesema dawa ya kutatua tatizo la uhaba wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa hapa ni wajasirimali kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kupenya soko la ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, Aprili 26, 2023 na Mkurugenzi wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido), Shome Kibende aliyemwakilisha Waziri wa Viwanda, Ashatu Kijaji, kati kongamano la wajasiriamali wachanga, wadogo na kati (MSMEs) lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited

Kongamano hilo limedhaminiwa na Benki ya CRDB, Kampuni ya usafirishaji ya DHL, Benki ya Stanbic, Benki ya NMB, Clouds Media na Ukumbi wa mikutano wa Dome.

Shome amesema iwapo wajasiriamali watachangamkia fursa mbalimbali zilizopo zitawasaidia kupata soko la nje katika kukuza biashara zao.

“Wajasiriamali hakikisheni bidhaa zenu ziwe bora, hakikisheni mnazitumia fursa za soko la Afrika, Afrika Mashariki na nje. Kitakachotuwezesha ni bidhaa bora bila hivyo hatuwezi kushindana katika soko.

“Tuzingatie pia afya ya binadamu ni muhimu lakini pia ni njia bora itakayotuwezesha kushindanisha bidhaa zetu na zile za wengine, itakayokuwa bora ndiyo itapendwa na kununuliwa” amesema Shome.

Amewapongeza Kampuni ya Mwananchi kwa kuandaa  kongamano hilo kwa kushirikina na taasisi nyingine zenye utaalamu na mchango katika maeneo tofauti kujadili fursa ili kuwezesha mazingira bora yatakayoinua mazingira ya viwanda vidogo na vya kati.

“Mbinu na ubunifu zaidi katika kukuza kampuni ni mambo ya kuzingatiwa kwa sasa. Tutumie fursa hii katika kongamano hili kujadili na kutatua fursa ili tukitoka hapa tuwe na maazimio mazuri yatajayotusaidia kukuza sekta yetu ya wajasiriamali,” amesema Shome.