Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madhara ya dhambi kwenye maisha yako

Bwana yesu asifiwe, naitwa Mwalimu George Mbwambo kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania- Usharika wa Buza, Dar es Salaam. Nikukaribishe katika mahubiri ya siku ya leo.

1 Yohana 3:4; Kila atendaye dhambi afanya uasi kwa kuwa dhambi ni uasi, unaposoma katika mistari hii unaona Biblia ikizungumzia kuwa dhambi ni uasi, yaani kwenda kinyume na maagizo ya Mungu. Yapo maagizo ambayo Mungu ameyatoa kwa wanadamu anahitaji wayafuate na wanapoacha kutii maagizo yake (Amri) wafanya dhambi na yapo madhara ambayo wanaweza kuyapata kwenye maisha yao.

Warumi 6:23b kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; katika mstari huu unatuonyesha matokeo au mshahara wa dhambi kuwa ni mauti. Mauti maana yake ni roho ambayo inaweza kumuua mtu au kuua baadhi ya vitu kwenye maisha yake, mfano biashara, ndoa, kazi, mahusiano nk., hivyo basi dhambi inaalika roho ya mauti kwenye maisha ya mtu. Katika kuliangalia hili tuangalie kwa mifano ifuatayo:


Adamu na mke wake

Mwanzo 2:16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,

17 Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Mwanzo 3 :17,19b Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 19b kwa jasho la uso wako utakula chakula.

Unaposoma mistari hii unaona Mungu akitoa amri au maagizo ya namna watakavyoishi Adamu na mkewe katika bustani ya Edeni, lakini Adamu na mkewe hawakutii maagizo ya Mungu, maana yake walifanya dhambi. Katika hili yapo madhara waliyapata, nayo ni kama ifuatavyo:


Kuishi maisha magumu ambayo Mungu hakuwapangia mwanzoni

Mwanzo 3:19b; Kwa jasho la uso wako utakula chakula. Mungu hakumpangia mwanadamu kuishi maisha ya tabu, lakini mlango wa dhambi ulisababisha maisha yakabadilika na kuwa ya tabu, ndiyo maana nakwambia kwamba dhambi ni mbaya, ina kawaida ya kubadilisha aina ya maisha mazuri ambayo Mungu alikuandalia uyaishi duniani, jambo la muhimu sana ni kutubu na kuamua kuacha dhambi ili uyaishi yale maisha ambayo Mungu aliyaandaa kwa ajili yako. Kingine ninachotaka ufahamu Adamu na mkewe walipofanya dhambi ilileta madhara pia kwa uzao wao unaofuata, kwa hiyo dhambi unayoifanya sasa inaweza kuleta madhara kwako na kwa uzao wako pia, ndiyo maana nasisitiza kuwa dhambi ni mbaya.


Kuupoteza uwepo wa Mungu kwenye maisha yao

Mwanzo 3:9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, uko wapi? Kabla ya dhambi Mungu alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Adamu na mkewe na walikuwa wakifunikwa na uwepo wa Mungu siku zote, lakini baada ya dhambi uwepo wa Mungu uliondoka kwenye maisha yao. Dhambi inaweza kukutoa kwenye nafasi ambayo Mungu amekupa, lakini pia dhambi inaweza kukuondolea uwepo wa Mungu kwenye maisha yako ya kila siku.

Kumbuka kuwa ili ufanikiwe kwa jambo lolote unalolifanya lazima uwepo wa Mungu uhusike, yaani Mungu awe pamoja na wewe akusaidie.Shetani anapokubembeleza ufanye dhambi anachotaka akutenge na uwepo wa Mungu ili ayavuruge maisha yako.


Mfano 2; Ahabu na mkewe Yezebeli

1 Wafalme 21 habari hii ni Habari ya Mfalme Ahabu ambaye alikuwa amelitamani shamba la Nabothi akumuomba amuuzie, lakini Nabothi alikataa. Mke wa Ahabu, Yezebeli aliandaa taarifa ya uongo kwamba Nabothi amemtukana Mungu hivyo anastahili kuuawa na kweli alifanikiwa kufanya dhambi hiyo ya kumuua Naboth. Baada ya hayo Mungu alimuadhibu Ahabu na Yezebeli, mkewe.

1 Wafalme 21:18 Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu katika Samaria; yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ndiko alikoshukia ili alitamalaki. 19 Ukamwambie, ukisema, Bwana asema hivi, je, umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia kusema, Bwana asema hivi,mahali mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.


Mfano 3 Kaini

Mwanzo 4:8 Kaini akamwambia Habili nduguye, twende uwandani. Ikiwa walipokuwa uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamuua.

Habari hii ni ya Kaini ambaye alimuonea ndugu yake wivu baada ya kuona kuwa ndugu yake amemtolea Mungu sadaka na sadaka yake imepokelewa. Katika maisha ya kila siku wapo watu ambao wana roho ya wivu, wakiwaona watu wengine wanafanikiwa wanatamani kuwarudisha nyuma. Omba Mungu atakuinua na wewe. Mungu alimwambia Kaini ukitenda vyema utapata kibali.

Mungu akubariki sana

Mwalimu George Mbwambo

Anapatikana: 0788873267