Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sera ya Taifa ya Bima yaja

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande

Muktasari:

  • Sera ya Taifa ya Bima itaweka mfumo madhubuti wa usimamizi wa masuala ya bima nchini, katika kuelekea BIma ya Afya kwa Wote.

Dodoma. Serikali imesema inaendelea kuyafanyia kazi maoni ya wadau wa sekta ya bima nchini ili kuboresha rasimu Sera ya Taifa ya Bima, inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza mchango wa sekta ndogo ya bima katika pato la Taifa.

Hayo yamesemwa leo Mei 14, 2025 na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande wakati akijibu swali la Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Dk Oscar Kikoyo ambaye alihoji ni lini Serikali itatunga Sera ya Taifa ya Bima.

Akijibu swali hilo, Chande amesema serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wengine inaendelea na zoezi la kuandaa Sera ya Taifa ya Bima ya mwaka 2025.

Amesema lengo ni kuweka mfumo madhubuti wa usimamizi wa masuala ya bima nchini, ikiwa ni pamoja na namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali ili kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza mchango wa sekta ndogo ya bima katika pato la Taifa.

”Kwasasa, wizara imekusanya maoni ya wadau wa sekta ya bima na inaendelea kuyafanyia kazi maoni yaliyotolewa ili kuboresha rasimu hiyo,” amesema.

Katika swali la nyongeza, Dk Ishengoma ameshauri Serikali kuharakisha mchakato wa kutunga sera hiyo ili kunusuru maisha ya Watanzania wanaokabiliwa na majanga, hasa majanga ya barabarani.

Akijibu swali hilo, Chande ameshukuru kwa ushauri huo na kwamba wanauchukua kwa ajili ya kwenda kuufanyia kazi.

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina amesema watumiaji wa bima wamefikia milioni nane na makusanyo ya bima ni zaidi ya Sh900 bilioni kwa mwaka.

“Je ni kwanini Serikali inaruhusu udanganyifu unaoendelea kwa baadhi ya wafanyabiashara kudai fidia na baadaye bidhaa hizo zilizolipiwa fidia kwenda kuuzwa tena na hivyo kusababisha wananchi kupata madhara makubwa,” amehoji.

Akijibu swali hilo, Chande amesema hilo ni suala la kulifuatilia, kulichukua na kwenda kulifanyia kazi na kama udanganyifu huo upo wataufanyia kazi na sheria itachukua mkondo wake.