Sekta binafsi yataka serikali iingilie kati Reli ya Tazara

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula
Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea kufanya mageuzi ya kiuchumi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula ameshauri ni muhimu kugeukia Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) ambayo kwa muda mrefu imekosa ufanisi wa kiutendaji.
Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 1,860, ikianza kazi yake mwaka 1976 ilikusidiwa iwe na uwezo wa kusafirisha mizigo tani milioni tano kwa mwaka lakini hadi sasa inasafirisha chini ya tani milioni moja.
“Ufanisi wake umekuwa mdogo mpaka leo yanasafirisha chini ya tani milioni moja kwahiyo tunakuomba Rais ikukupendeza uangazie na maeneo mengine na hili jambo tuko na wewe bega kwa bega,” amesema.
Hayo amebainisha Dar es Salaam leo, Juni 9, 2023 kwenye ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), ambapo mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa mwenyekiti wa Baraza hilo Rais Samia Suluhu Hassan.