Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samia: Ni aibu Afrika kulia njaa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mjadala wa masuala ya kilimo na vijana wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Septemba 7, 2023. Picha na Ikulu

Muktasari:

  • Rais, Samia Suluhu Hassan amesema ni aibu nchi za Afrika kuwa walalamikaji juu ya ukosefu wa chakula wakati asilimia 65 ya ardhi inayofaaa kwa kilimo duniani iko katika bara hilo.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ni aibu nchi za Afrika kuwa walalamikaji juu ya ukosefu wa chakula wakati asilimia 65 ya ardhi inayofaaa kwa kilimo duniani iko katika bara hilo.

Hivyo amelitaka jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF), kutoka na suluhu ya changamoto ya chakula na mifumo ya chakula.

Ametoa kauli hiyo wakati akihutubia jukwaa hilo leo Septemba 7, 2023 wakati marais mbalimbali wa nchi za Afrika walipokutana kujadili juu ya nini kifanyike kuboresha mifumo ya chakula Afrika.

Samia amesema licha ya rasilimali zilizopo Afrika, imebaki kuwa wakalamikaji badala ya kutafuta suluhisho kuelekea njia inatakayoleta mapinduzi ya uchumi wa kijani.

"Inakadiriwa zaidi ya watu milioni 283 wa Afrika wanalala na njaa wengine wanapata utapiamlo na magonjwa yanayotokana na lishe na wapo wanaokufa kwa kukosa chakula, ni aibu na haitakiwi hata kidogo," amesema Samia.

"Tuko hapa AGRF, washirika wa maendeleo, sekta binafsi wasomi na wataalamu kutoka Afrika na duniani kujadili kadhia hiyo, kubadilishana uzoefu namna ya kuendesha minyoyoro ya thamani ya bidhaa za kilimo na kujadili mipango ya kuimarisha usalama wa chakula na ustawi wa kiuchumi barani Afrika," amesema Samia.

Amesema ili kufikia malengo tarajiwa, viongozi wa Afrika hawana budi kufanya thathmini ya vipaumbele vyao na kuvioanisha na mahitaji ya sasa katika muktadha wa kidunia.

"Hii ni kuelekea maguezi tunayoyataka katika sekta ya kilimo kufika katika Afrika tunayoitaka," amesema Samia.