Samia atua Mwanza kushiriki tamasha la utamaduni wa Mtanzania

Muktasari:
- Rais Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza kwa helkopta maalum kwa ajili ya kufunga tamasha la utamaduni wa Mtanzania linalofanyika katika viwanja vya Msalaba Mwekundu vilivyopo karibu na makumbusho ya Bujora wilayani Magu mkoani humo.
Mwanza. Rais Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza kwa helkopta maalum kwa ajili ya kufunga tamasha la utamaduni wa Mtanzania linalofanyika katika viwanja vya Msalaba Mwekundu vilivyopo karibu na makumbusho ya Bujora wilayani Magu mkoani humo.
Rais Samia amepokewa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel.
Tamasha hilo lilianza jana Jumanne Septemba 7, 2021 na linatarajiwa kuhitimishwa leo huku lengo lake likiwa kudumisha, kurithisha na kuutangaza utamaduni wa makabila ya Tanzania.
Mwananchi Digital imepita katika maeneo ya Buzuruga, Igoma na National na kushuhudia wananchi wakiwa wamesimama pembeni mwa barabara tayari kumpokea kiongozi mkuu huyo wa nchi.
Katika tamasha hilo zaidi ya viongozi wa kimila kutoka makabila zaidi ya 120 wamehudhuria huku likisindikizwa michezo ya jadi, ngoma na vyakula vya asili.