Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samia amulika madereva wa 'Ambulance'

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza leo Septemba 15, 2023 wakati akizindua jengo la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini katika ziara yake ya siku nne mkaoni Mtwara.

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu ameonya matumizi mabaya ya magari ya kubebea wagonjwa mahututi (ambulance), kwa baadhi ya madereva ambao anasema huyatumia kusafirishia magendo.

Mtwara. Rais Samia Suluhu Hassan ameonya matumizi mabaya ya magari ya kubebea wagonjwa mahututi yanayofanywa na baadhi wa madereva ambao anasema wamekuwa wakiyatumia kusafirisha magendo.

Akizungumza leo Septemba 15, 2023 wakati akizindua jengo la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini katika ziara yake ya siku nne mkaoni hapa, Rais amesema kuwa hataki kusikia gari zikiwa zimepakia magendo huku zikipita barabarani mithiri ya kuwa na mgonjwa. 

“Unakuta dereva anapita barabarani kumbe amepakia magendo ambapo ndani yake kuna mzigo haramu, ikitokea hivyo dereva na aliyempa mali na anayemsimamia wote mnakwenda, sawa? Gari hizi zitumike kwa kazi iliyokusudiwa,” amesema Rais Samia.

Aidha Rais amesisitiza suala la usafi katika jengo hilo jipya katika hospitali hiyo ya kanda, ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya Sh15 bilioni, na kwamba in uwezo wa vitanda 100, huku ikitarajiwa kuhudumia wagonjwa kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. 

“Niwapongeze, hongereni kwa kazi nzuri, jambo kubwa hapa ni usafi wa hospitali, haipendezi unafika pale unaona vumbi linaning’inia, libakie safi hivi hivi siku zote, niwasihi wanaosafisha hospitali hii wapelekwe kozi maalum kama ile wanayoisoma wanaofanyakazi katika mahoteli” amesema na kuongeza. 

“Ili wajue jinsi ya kutandika vitanda na kuweka hospitali katika hali ya usafi, ikiwezekana...hili jengo ni refu, tafuteni wale wanaosafisha vioo kwa kutumia ngazi ili usafi uweze kufanyika kwa ustadi zaidi,” amesema Rais Samia.

“Tumeweka vifaa vya kisasa kila kitu hapa ni cha kisasa yaani ni vifaa vyenye uwezo, tumeleta huduma kwa watu wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ili wananchi wenye magonjwa makubwa waweze kuja hapa wapate huduma nzuri na bora,” amesema Rais Suluhu.

“Unajua Mwenyezi Mungu amewateua nyie mfanye kazi hapa ya kuokoa maisha ya watu pamoja na changamoto zote za kiafya zilizopo ndani ya mkoa wa Mtwara, mkumbuke kuwa kazi yenu ni kuokoa maisha ya watu hatutaki starehe, lazima kuwe na vifaa muhimu na wakuu wa idara wawe na vifaa binafsi kama vishkwambi,” amesema Rais Suluhu.

Uzinduzi wa hospitali hiyo, unaifanya Tanzania kuwa na hospitali za hadhi hiyo saba, ambapo zingine ni Hospitali ya Lugalo ambayo ilipandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda, pia ipo Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando.

Pia Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Benjamin Mkapa, na hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato