Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samia amuagiza Majaliwa kuunda kamati kuwachunguza Polisi mauaji Mtwara

Rais Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuunda kamati huru kuchunguza tuhuma za mauaji mkoani Mtwara yanayodaiwa kufanywa na askari polisi.

Magu. Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuunda kamati huru kuchunguza tuhuma za mauaji mkoani Mtwara yanayodaiwa kufanywa na askari polisi.

Akizungumza leo Ijumaa Februari 4, 2022 wakati akiwa Magu akielekea katika sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya CCM mkoani Mara zitakazofanyika kesho, Rais Samia amekosoa polisi kuunda kamati ya kujichunguza wenyewe baada ya tukio hilo.

"Kuna mauaji yametokea Mtwara na kwa taarifa zilizopo ni Polisi ndio lililofanya mauaji. Taarifa niliyonayo ni kwamba Polisi wameunda kamati ya kufanya uchunguzi halafu walete taarifa."

"Haiwezekani Jeshi lifanye mauaji halafu jeshi lichunguze lenyewe” amesema Rais Samia nakuongeza.

Nimemuelekeza Waziri Mkuu aunde kamati nyingine iende ikafanye uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi halafu watuletee taarifa lakini wakati huohuo nataka Jeshi lako lijitafakari waone kama kinachotokea ni misingi ya Jeshi la Polisi, "amesema.

Katika ufafanuzi wake Rais Samia amesema,"kwa hiyo tutasubiri taarifa ya kamati huru itakayoundwa na Waziri Mkuu ituletee taarifa tulinganishe na ile ya Jeshi la Polisi tuonee taarifa mbili zinasemaje tuchukue hatua muafaka."

Hivi karibuni askari saba wa Jeshi la Polisi walipandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauaji ya mfanyaniashara wa madini mkoani Mtwara huku wa nane aliyekabiliwa na tuhuma hizo akijinyonga alipokuwa mahabusu.