Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la utekaji laibuka bungeni

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akijibu maswali bungeni jijibi Dodoma leo Jumatano Februari 7, 2024.

Muktasari:

  • Hatimaye suala la utekaji wa watu limetua bungeni baada ya Mbunge wa Nyang’hwale, Hussein Amar kuihoji Serikali ina mpango gani wa haraka kuzuia matukio hayo katika Jiji la Dar es Salaam.

Dodoma. Mbunge wa Nyang’hwale, Hussein Amar ameihoji Serikali ina mpango gani wa haraka kuzuia utekaji unaoendelea katika Jiji la Dar es Salaam.

Miongoni mwa matukio matano ya watu kutekwa na kutoweka katika mazingira ya kutatanisha yalitokea mwaka 2023, limo la kutekwa mfanyabiashara Mussa Mziba (37), aliyekuwa akimiliki Kampuni ya Mziba Empire Investment Ltd ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Tukio lingine ni la kutekwa kwa aliyekuwa mfanyabiashara na fundi wa simu katika eneo la Kariakoo Dar es Salaam, Innocent Elias Liveti (34) maarufu Macheni.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumatano Februari 7, 2024, Amir amehoji Serikali ina mpango gani wa haraka kuzuia utekaji unaoendelea ndani ya jiji la Dar es Salaam na kupoteza maisha ya watu.

Amesema amehoji hilo kwa sababu utekaji huo unaendelea kila kukicha.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema wanafuatilia kwa karibu matukio yanayoendelea kutokea katika Jiji la Dar es Salaam kwa madhumuni ya kudhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria wanaohusika na hicho kinachoitwa utekaji.

Matukio kama hayo yamesharipotiwa Simiyu, Shinyanga, Singida, Mara na Kigoma na wiki iliyopita Gazeti la Mwananchi liliandika kwa kirefu likibainisha matukio kadhaa ya watu waliopotea wakiwemo waliotekwa.