Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo laibuka bungeni

Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma akiomba mwongozo wa Spika kwa kutumia kanuni ya Bunge ya 76 leo Jumatatu Juni 24,2024 bungeni jijini Dodoma.

Muktasari:

  • Sakata la mgomo wa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo limetinga bungeni huku Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu akisema Serikali itatoa taarifa rasmi.

Dodoma. Sakata la mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, jijini Dar es Salaam limeibuka bungeni, huku Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu akisema Serikali itatoa taarifa baada ya kikao kati yake na kamati ya wafanyabiashara kukamilika.

Sakata hilo limeibuka leo Jumatatu Juni 24,2024 bungeni jijini Dodoma baada ya Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma kuomba mwongozo wa Spika kwa kutumia kanuni ya Bunge ya 76.

“Naomba nianze kutumia mwongozo kwa kutumia lugha ya Dar es Salaam, wanasema kuwa kazini kwako kuna kazi na kwamba kumekuwa na kipeperushi ambacho kinatokea mitandaoni kuwa kuanzia Jumamosi kuhusiana na wafanyabiashara wa Kariakoo na sehemu nyingine nchini kufunga maduka Jumatatu ambayo ni leo.

"Tunapozungumza sasa hivi, Kariakoo imefungwa hakufanyiki biashara na sisi wabunge kuna mambo ambayo tuliya-‘rise’(tuliyaibua) katika michango yetu.  Tunatambua kuwa kamati ya wafanyabiashara ipo hapa kufanya mazungumzo na Serikali kutatuliwa matatizo yao.” amesema.

Ameomba mwongozo kuhusu kauli ya Serikali kuhusiana kugoma kwa wafanyabiashara wa Kariakoo na kwamba watu wao kutoka vijijini wamekwenda Kariakoo kufuata mahitaji wamekuta Kariakoo maduka yafungwa.

“Wengine hawana nauli wanaanza tena kuomba tena kwetu wabunge, nilikuwa naomba mwongozo wako ni nini kauli yako kuhusiana na wafanyabiashara kufunga maduka,”amesema.

Akijibu mwongozo huo, Zungu amesema anafahamu juzi Musukuma alizungumzia suala hilo na kwamba Serikali na wafanyabiashara wanakutana na kwamba taarifa kamili wataipata baada ya kikao hicho kumalizika.

Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao, wanalamikia kuchoshwa na vitendo wanavyofanyiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Leo Jumatatu, Juni 24, 2024 Mwananchi imeshuhusdia wafanyabiashara katika eneo hilo wakiwa wamekaa nje, huku maduka yao yakiwa yamefungwa.

Biashara pekee inayoendelea ni ile inayofanywa na wafanyabiashara ndogondogo 'machinga' katika mitaa mbalimbali sokoni hapo.