Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruwasa yamaliza kero ya maji Sengerema

Muktasari:

  • Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza imedhamilia kumaliza kero ya maji katika Kijiji cha Kamisa baada ya kukamilika kwa  mradi wa maji wa kijiji hicho.


Buchosa. Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza imedhamilia kumaliza kero ya maji katika Kijiji cha Kamisa baada ya kukamilika kwa  mradi wa maji wa kijiji hicho.

Mradi huo ulioanza kutekelezwa Machi 2021 kwa gharama ya Sh225milioni una lengo la kutoa  huduma kwa wakazi 400 wa kijiji hicho.

Kaimu meneja wa  RUWASA Wilaya ya Sengerema, Venslaus Blaise amesema kukamilika kwa mradi huu kumeondoa tatizo la maji kwenye Kijiji cha Kamisa.

Amesema kwa Wilaya ya Sengerema hali ya huduma ya maji wilayani humo kwa upande wa vijiji, imefikia asimilia 57 ya Wananchi wapatao 628,632 kuishia Juni mwaka 2021.

Bleise amesema kwa miradi ya maji inayotarajia kutekelezwa mwaka wa fedha 2021/2022 itakapokamilika  wanatarajia kufikia asimilia kati ya 75 hadi 85 mwezi Juni 2022.

" Miongoni mwa vyanzo vya fedha za kutekeleza miradi ya maji ni mpango wa malipo baada ya matokeo, ambao umetekeleza mradi wa maji Kamisa" amesema Bleise.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo amewataka Wakala wa maji Vijijini( RUWASA) kuhakikisha Miradi yote maji inayotekelezwa vijijini ikamilike kwa wakati na isiwe chini ya kiwango.

Shigongo amesema kwa kukamilika mradi wa maji wa Kamisa kumeleta  faraja kwa wananchi hivyo miradi inapokamilika na kutoa maji Wananchi wanapata huduma inawapunguzia mzingo wa kutafuta maji kwenye madimbwi.

Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kamisa Anna Tibalila amesema kukamilika kwa mradi maji kumewaondolea adha kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Amemshukuru mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo kwa kufuatia kwa kina hadi mradi huu kukamilika nakutoa huduma ya maji.