Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruto anavyochakazwa kwa ‘skendo’ uchaguzi ukikaribia

Mgombea urais wa United Democratic Alliance (UDA), William Ruto

Muktasari:

Kasi ya kufukua makaburi ya skendo za wagombea inaongezeka kadiri tarahe ya uchaguzi inavyosogea jirani.

Kasi ya kufukua makaburi ya skendo za wagombea inaongezeka kadiri tarahe ya uchaguzi inavyosogea jirani.

Yote yafukuliwe ila ya mgombea urais wa United Democratic Alliance (UDA), William Ruto, yamekuwa mengi.

Ruto anaandamwa na kashfa nyingi. Kuanzia kashfa za rushwa na ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi za umma na kujinufaisha binafsi hadi tabia binafsi za ugomvi. Yote hayo yanaibuliwa kwa nguvu kabwa, wakati Wakenya wakisuburi Agosti 9, ifike waweze kufanya uamuzi.


Uporaji ardhi

Umiliki wa ardhi ambayo ipo hoteli yake ya Weston, Barabara ya Lang’ata, Nairobi, unakumbushiwa sasa hivi. Ruto anadaiwa kujipatia kiwanja hicho kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA), kwa njia za kifisadi.

Maelezo ambayo Ruto amekuwa akitoa kuhusu umiliki wa kiwanja hicho ni kuwa yeye alinunua ardhi kihalali kutoka kwenye taasisi iliyopewa umiliki na kamishna wa ardhi.

Hata hivyo, rekodi zinaonyesha kuwa taasisi mbili ambazo zilitambuliwa kama wamiliki wa ardhi husika ni Priority Limited na Monene Investments Limited.

Kisha, taasisi zote hizo zinatumia anuani moja, Sanduku la Posta 62860, Nairobi. Na anuani hiyohiyo ndiyo inayotumiwa na kampuni ya kilimo ya Koilel Farm Ltd, ambayo wakurugenzi wake ni mke wa Ruto, Rael Kimeto Chebet na mtoto wao wa kiume, Nicholas Ruto.

Kauli ya Ruto kuwa alinunua ardhi kutoka kwa taasisi iliyomilikishwa na kamishna wa ardhi, halafu taasisi zilizoandikishwa kuwa wamiliki wa kiwanja baada ya KCAA kutumia anuani moja na kampuni nyingine ambayo Naibu Rais huyo anahusika nayo, imekuwa sababu ya kashfa hii ambayo ilikuwa imeshazikwa, kaburi lake kufukuliwa upya.

Maelezo zaidi kuhusu kashfa hiyo ni kwamba kiwanja hicho cha Barabara ya Lang’ata, kilibadilishwa umiliki Januari 5, 1998, siku moja baada ya Rais wa Pili wa Kenya, Daniel Moi, kuapa muhula wake wa mwisho. Kilibadilishwa pia wakati wa hekaheka za uchaguzi mwaka 2002.

Juni 2007, nchi ikiwa kwenye joto lingine la uchaguzi, ndipo umiliki wa ardhi hiyo ulihamishiwa rasmi kwa Weston Hotels. Inajengwa hoja kuwa Ruto alikuwa akingoja kipindi mtazamo wa nchi upo kwenye uchaguzi ndipo alipofanya uhamishaji wa umiliki kwa kushirikiana na maofisa wa ardhi.

Weka kando mgogoro wa ardhi ya Weston Hotels; rejea kampuni ya Priority Limited, ambayo imetajwa kutumia anuani moja na kampuni ya kilimo ya Koilel Farm Ltd, inayomilikiwa na mke wa Ruto na mwanawe, Nicholas.

Kampuni hiyohiyo, Priority Ltd, ndiyo iliyohusika katika kasfa ya Msitu wa Ngong, ambayo mwaka 2004, Ruto alishitakiwa kwa kujimilikisha ardhi ya umma, kisha kuiuza kwa kampuni ya Kenya Pipeline Ltd kwa Shilingi za Kenya milioni 272 (Sh5.3 bilioni kwa sarafu ya Tanzania).

Katika kesi hiyo, Ruto alishitakiwa pamoja na aliyekuwa Kamishna wa Ardhi, Sammy Mwaita, vilevile Joshua Kulei, ambaye ni msaidizi wa zamani wa Rais Moi.

Vurugu za kisiasa mwaka 2007 na 2008, zilisababisha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Mwai Kibaki na Raila Odinga, walikubali kushirikiana kuongoza serikali. Ruto akiwa upande wa Raila, alikula ‘shavu’, akateuliwa kuwa Waziri wa Kilimo.

Baada ya Ruto kuingia baraza la mawaziri, anadaiwa kuingiza ushawishi na kufanya kesi ya uporaji wa Msitu wa Ngong, kupoteza uelekeo. Kuna kashfa ya shamba la ekari 2,500 lililopo Taifa Taveta. Mwanzoni kwenye kampeni zake, Ruto alisema kuwa alipewa ardhi ya shamba la Mata na mbunge wa zamani wa jimbo la Taveta, Basil Criticos. Ruto alisema, Criticos alikuwa na matatizo ya mkopo, yeye aliweza kumsaidia. Kwa shukurani, Criticos alimkatia kipande hicho cha ardhi.

Kauli hiyo iliibua ukosoaji wa kisheria. Alikosolewa kuwa akiwa Naibu Rais, kupokea zawadi hiyo ya shamba kutoka kwa Criticos ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma. Siku nne baada ya mdahalo, Criticos alijitokeza na kueleza kuwa Shamba la Mata lililopo Taifa Taveta, alimuuzia Ruto kwa kufuata taratibu zote za kisheria. Kauli ya Criticos kuwa alimuuzia, inakinzana na ya Ruto mwenyewe aliyoitoa Taveta.


Kashfa nyingine

Kashfa ya mahindi imeubuliwa upya. Januari 2009, ndipo kashfa ya mahindi iliwekwa kwenye uso wa jamii. Kipindi hicho Ruto alikuwa Waziri wa Kilimo.

Mwaka 2008, Serikali ya Kenya iliondoa kikwazo cha kuagiza mahindi. Awali, kulikuwa marufuku ya mahindi kuingizwa Kenya ili kuwezesha wakulima wa ndani kujidai na soko lao.

Kashfa inaanza kwenye maelezo kuwa Ruto akiwa na mgongano wa masilahi, kama Waziri wa Kilimo, alifanikisha kuondoa zuio la kuingizwa mahindi ndani, halafu yeye akawa mnufaika wa uingizaji wa nafaka hiyo.

Skendo ya Mahindi iliibuka kwa sababu baada ya ruhusa mahindi kuingizwa ndani kulikuwa na utaratibu wa kufutwa. Taasisi mbili za Serikali; Hifadhi ya Kimkakati ya Nafaka (SGR) na Bodi ya Taifa ya Mazao ya Nafaka Kenya (NCPBK), zilipaswa kupitisha vibali, kukagua na kupima mahindi kama yanafaa kwa matumizi.

Kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa kutosha, sio SGR na NCPBK peke yake, kulikuwa na makatibu wakuu wanne wa wizara ambao walitakiwa kusaini baada ya kujiridhisha kitaalamu kuwa mahindi husika na salama kwa Wakenya. Utaratibu huo ukiwa unafahamika na Ruto akiwa Waziri wa Kilimo, alikutwa na hatia kwenye Bunge la Kenya, ya kuingiza mahindi na kuuza kinyume na sheria na pasipo kufuata mtiririko uliowekwa.

Ruto, alimuuzia mahindi aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ikolomani, Bonny Khalwale, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge.