Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RPC Tabora afariki dunia akipatiwa matibabu Muhimbili

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Richard Abwao eni za uhai wake. Picha na Mtandao

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Richard Abwao amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime ameithibitisha Mwananchi leo Jumamosi, Julai 20, 2026 kuhusu kifo cha ofisa huyo alikuwa cheo cha Kamishna Msaidizi wa Mwandamizi.

“Ni kweli aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi Richard Abwao amefariki dunia leo 20.6.2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu,”

“Taratibu zingine mtajulishwa baadaye,” amesema Misime.

Enzi za uhai wake, Abwao amewahi kuhuduma katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu kabla ya kuhamishiwa mkoani Tabora.


Endelea kufuatilia Mwananchi