Ripoti kikosi kazi leo

Rais Samia Suluhu Hassan
Muktasari:
Ripoti ya kikosi kazi cha kupitia maoni ya wadau wa demokrasia inatarajia kukabidhiwa leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 kwa Rais Samia Suluhu Hassan
Dar es Salaam. Ripoti ya kikosi kazi cha kupitia maoni ya wadau wa demokrasia inatarajia kukabidhiwa leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 kwa Rais Samia Suluhu Hassan
Ripoti hiyo inasubiriwa kwa shauku na wadau mbalimbali wa demokrasia ambao wana shauku ya kupata suluhisho la mchakato wa Katiba mpya, uwanja sawa wa siasa na tume huru ya uchaguzi.
Kikosi kazi hicho kiliundwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili kupitia maoni ya wadau wa demokrasia waliokutana jijini Dodoma, Desemba 15 hadi 17 mwaka jana.
Kikao hicho kilifunguliwa na Rais Samia na baada ya kuundwa kilipewa jukumu la kupitia maoni 80 yaliyotolewa na wadau hao.
Machi 12 mwaka huu, Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho, Profesa Rwekaza Mukandala aliwaongoza wajumbe kuwasilisha taarifa yake kwa Rais Samia baada ya hapo, mkuu huyo wa nchi alisema kuanzia wakati huo kitakuwa kikiripoti kwake.