Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia: Demokrasia si matusi ni maoni

Rais Samia Suluhu Hassan

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema demokrasia si matusi ni maoni hivyo anayehubiri demokrasia lazima alinde utu na nafasi ya mtu.

Ameeleza hayo leo Jumatatu Septemba 11, 2023 katika mkutano maalumu wa baraza la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema maoni yanaweza kuwa mazuri na yakampendeza anayepewa au yasimpendeze.

 “Tunapozungumza demokrasia tunazungumzia utu wa mtu, nafasi ya mtu lazima viheshimiwe, wewe unayesimama kuzungumza demokrasia lazima ujue una mambo lazima uyaheshimu, kuna maoni na matusi sasa demokrasia si matusi demokrasia ni maoni."

"Maoni yanaweza kuwa mazuri yakampendeza unayempa,  yanaweza kuwa mabaya...,  lakini ni maoni umeyatoa unaposimama na kuvurumusha matusi kwa kivuli cha demokrasia kumkashifu mtu na dini yake kwa kivuli cha demokrasia hiyo siyo demokrasia huo ni utovu wa adabu."

“Demokrasia haina fomula moja, ni muhimu tunapofikiria hiyo katiba yetu mpya tujue demokrasia yetu itakwenda na mambo yetu ya ndani, mila zetu desturi zetu tunavyoendesha mambo kuna mambo hatuwezi kuyapokea kama yalivyo haiwezekani,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.