Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia awatakia kheri kidato cha sita

Muktasari:

  • Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetoa onyo kwa wadau mbalimbali wakiwamo wananchi kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na miongozo yote, ili kuwezesha mitihani hiyo kufanyika kwa ufanisi.

Dar es Salaam. Wakati leo Jumatatu, Mei 5, 2025 wanafunzi wa kidato cha sita na ualimu wakianza mitihani yao ya Taifa Rais  wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatakia heri.

Mitihani hiyo kwa kidato cha sita itahitimishwa Mei 26, 2025 huku ile ya ualimu itamalizika Mei 19, 2025. Hii ni kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).

Jana Jumapili, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohamed alisema watahiniwa 134,390 wa kidato cha sita wanatarajia kufanya mitihani hiyo.

Dk Mohamed alisema watahiniwa 10,895 wamesajiliwa kufanya mtihani wa ualimu na kati yao 3,100 ni wa ngazi ya stashahada na 7,795 ngazi ya cheti.

Leo Jumatatu, Rais Samia ametumia ukurasa wake wa kijamii kutoa salamu hizo akisema:”Ninawatakia kila la kheri wanangu wote wa kidato cha sita na ualimu ngazi ya Astashahada na Stashahada mnaoanza mitihani yenu ya kuhitimu leo. Hii ni hatua kubwa na muhimu katika safari yenu ya kielimu na kimaisha.”

“Serikali imefanya kazi kubwa kisera na kiuwekezaji katika sekta ya elimu ili muweze kuipata katika mazingira sahihi, na ninaamini mmeandaliwa na kujiandaa vya kutosha kwa mitihani hii. Mwenyezi Mungu awaongoze na kuwasimamia.”