Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia atoa kauli kuhusu hoja ya Katiba mpya

Rais Samia atoa kauli kuhusu hoja ya Katiba mpya

Muktasari:

  • Madai ya mara kwa mara ya Katiba Mpya yamemfanya Samia Suluhu Hassan kutoa kauli ya kwanza kuhusu suala hilo baada ya kujikuta mara tatu katika matukio tofauti anataja neno ‘Bunge la Katiba’ badala ya Bunge la Bajeti.

Dar es Salaam. Madai ya mara kwa mara ya Katiba Mpya yamemfanya Samia Suluhu Hassan kutoa kauli ya kwanza kuhusu suala hilo baada ya kujikuta mara tatu katika matukio tofauti anataja neno ‘Bunge la Katiba’ badala ya Bunge la Bajeti.

Baada ya kuingia Ikulu Machi 19 mwaka huu, wadau mbalimbali wamekuwa kushinikiza kwa mkuu huyo wa nchi kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya, ambao ulikwama katika hatua ya kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa mwaka 2014.

Baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani aliamua kuiweka kando akisema haikuwa kipaumbele kwake.

Wadau wa Katiba wameeleza matumaini kwa Rais Samia kwa kuwa ndiye alikuwa Makamu mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba lililopitisha Katiba Inayopendekezwa.

Hata hivyo, jana Rais Samia alisema wanaoshinikiza suala hilo wasubiri kidogo.

Mazingira ya Rais Samia kutumia msamiati huo yalichagizwa na msisitizo wake kwa mawaziri kufanya kazi kwa bidii katika maeneo mbalimbali ya nchi.

“Sisi ni watumishi wa Watanzania na nitakuwa na kipimo cha mabega, mabega yakizidi kupanda juu najua huyo siyo mtumishi, nataka niwaone huku na huko baada ya Bunge la Katiba,” alisema akimaanisha Bunge la Bajeti linaloendelea kwa sasa mjini Dodoma.

Baadaye akaongeza: “Kwa sasa mko kwenye Bunge la Katiba, ahaa! Hivi nina maradhi gani na Katiba? Nadhani wamenisukuma sukuma sana, Katiba, Katiba lakini wasahau kidogo,” alisema Rais Samia wakati wa hotuba yake ya kuapisha mawaziri na manaibu 16 walioteuliwa kupitia mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri.

Hii ilikuwa mara ya pili Rais Samia kujikuta akitaja neno Bunge la Katiba badala ya Bunge la Bajeti linaloendelea kwa sasa mjini Dodoma.

Rais Samia alikuwa makamu mwenyekiti katika bunge hilo lililoanza Februari 18, 2014 kabla ya kumaliza vikao Oktoba 2 na kukabidhi Katiba Inayopendekezwa Oktoba 8, 2014 kwa Rais mstaafu Kikwete na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohamed Shein.

Kabla ya bunge hilo lililoongozwa na Hayati Samuel Sitta akisaidiwa na Samia, Tume ya Kukusanya na Kuratibu maoni kuhusu Mabadiliko ya Katiba chini ya Mwenyekiti wake Jaji Joseph Waroba ilianza kukusanya maoni ya wananchi Julai 2, mwaka 2012 kabla ya hatua nne zilizofuata.

Baada ya kumaliza kukusanya maoni ya wananchi na kupata rasimu ya kwanza, tume hiyo ilirejea kukusanya maoni tena kupitia Mabaraza ya Katiba kabla ya kuandaa rasimu ya pili iliyowasilishwa katika Bunge hilo Maalumu lililomtambulisha na kumpatia umaarufu zaidi Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa ratiba, Serikali chini ya Rais Kikwete ilitangaza kwamba Katiba hiyo Inayopendekezwa ingepigiwa kura ya Ndiyo au Hapana na Watanzania wote wenye umri wa kupiga kura kupitia kura ya maoni Aprili 30, 2014 lakini mipango hiyo haikuwezekana.

Vyama vya siasa vimekuwa mara kwa mara vikipigia chapuo mchakato huo uanze upya, vingine vikitaka urejee hatua ya rasimu ya Warioba.

Juzi, Baraza la Vijana wa Chadema liliwasilisha pendekezo la kumtaka Rais Samia kurejesha mchakato wa Katiba Mpya katika hatua ya rasimu ya pili iliyodaiwa kuondolewa vifungu muhimu na bunge hilo ili Watanzania waweze kupata Katiba inayogusa maoni yao ya msingi.

Katika mazingira tofauti, jana pia Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba naye licha ya kusisitiza suala la kurejesha mchakato wa Katiba Mpya, alimshauri Rais Samia kujiwekea lengo la kufuata misingi ya demokrasia, kukuza uchumi na kutenda haki.