Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais samia ateuwa wenyeviti wawili

Muktasari:

  • Siku moja kabla ya kuwasilishwa bungeni kwa bajeti ya Wizara ya Maji, Rais Samia afanya uteuzi wa wenyeviti wawili wa bodi akiwemo wa Mfuko wa Taifa wa Maji.

Dar es Saalaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua kwa mara nyingine Profesa Elifas Bisanda kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Unesco ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha uongozi wake.

Profesa Bisanda anaendelea kushikiria usukani wa kuiongoza bodi ya tume hiyo ambayo ina jukumu la kusimamia amani, usalama na utamaduni wa nchi ikifanya kazi kwa ukaribu na Shirika la Kimataifa la Elimu, Utamaduni na Teknolojia (UNESCO).
Taarifa ya uteuzi iliyotolewa Mei 9 imeonyesha kumgusa pia Abdallah Mkufunzi ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Maji.
Mojawapo ya majukumu ya mfuko huu ni kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.
Mfuko wa taifa wa maji ulianza kufanya kazi nchini mwaka 2016 kwa lengo la kuhakikisha sekta ya maji ina kuwa na uhakika wa fedha zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhuru Yunus, uteuzi huo ulianza Mei 5 mwaka huu.