Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia apangua mawaziri, makatibu wakuu

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri na makatibu wakuu katika wizara mbili.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya mawaziri katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii sambamba na makatibu wakuu wa wizara hizo.

Mabadiliko hayo yamefanywa leo Februari 14, 2023 kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus teuzi hizo zinaanza mara moja ambapo wateule wataapishwa Februari 15, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amemuhamisha Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Aidha amefanya mabadiliko kwa kumtoa Balozi Pindi Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akihamishiwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu, amemuhamisha Dk Hassan Abbas Said aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye anachukua nafasi ya Profesa Eliamani Sedoyeka.

Rais amemuhamisha Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yakub akichukua nafasi ya Dk Abbas.

Kabla ya uteuzi huo Yakub alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Profesa Sedoyeka aliyekuwa Katibu Mkuu Maliasili na Utalii miezi saba tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akitoka kuwa mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha na sasa atasubiri kupangiwa kazi nyingine.