Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia anayaishi maridhiano – Dk Biteko

Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa ni muumini namba moja wa maridhiano nchini na haishii katika kusema tu bali anatekeleza kwa vitendo huku nia ikiwa ni kuhakikisha kunakuwa na umoja na amani nchini.

Dk Biteko ameyasema hay oleo Jumapili, 10 Disemba, 2023 wakati wa Misa Maalum ya Kutabaruku Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Lukajange, Dayosisi ya Karagwe iliyofanyika wilayani Karagwe, Mkoa wa Kagera.

Misa hiyo maalum imehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwasa.

"Rais Samia anasema kila mara kuwa hii nchi ni yetu sote, anatuasa mara nyingi kuwa wewe kama ni CCM mpende mpinzani, na mpinzani mpende CCM, tuungane pamoja tusukume nchi yetu mbele.

“Na hakuishia hapo tu, akaunda Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano ambayo imejumuisha makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa kutoka vyama mbalimbali na viongozi wa dini ili kuwe na muafaka nchini, tujenge Tanzania bora kwa ajili yetu na vizazi vijavyo," Amesisitiza Dk Biteko.

Ameongeza kuwa, Rais Samia amekuwa muumini wa maridhiano si kwa kuigiza bali kwa dhati ya moyo wake na ameonyesha mifano mbalimbali ya maridhiano ikiwemo kuwa Mgeni rasmi katika Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Moshi na hicho ni kiashirikia kikubwa cha kuonyesha kuwa anataka umoja na amani nchini.

vilevile, Dk Biteko ameendeelea kusisitiza kuwa Serikali inaunga mkono madhehebu ya dini na shughuli za kidini nchini na ndiyo maana imeendelea kutoa uhuru wa kuabudu kwa kila Mtanzania.

Katika hatua nyingine, Dk Biteko ametaka viongozi mbalimbali nchini kufanya kazi na watu wanaowaunga mkono na wasiowaunga mkono kwani wajibu wao ni kuwahudumia wananchi wote.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo amesema, miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa katika sekta mbalimbali ikiwemo za  nishati, miundombinu, afya ili kuelekea katika Tanzania tunayoitaka.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana amempongeza Askofu Benson Bagonza kwa uongozi mzuri katika Dayosisi ya Karagwe na ujenzi wa Kanisa Kuu jipya katika Dayosisi hiyo.

Pia amewapongeza Mashemasi watano katika Dayosisi hiyo ambao wamepata Uchungaji.

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa  amepongeza pia ujenzi wa Kanisa hilo Kuu na pia amempongeza Askofu Bagonza kwa kufanya kanisa katika Dayosisi hiyo kuzidi kusonga mbele.  Pia ameahidi kushirikiana nao katika kujenga Dayosisi hiyo.

Askofu wa Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza amemshukuru Rais Samia kwa kusimamia  suala la maridhiano kwa makundi yanayoonyesha kukinzana huku akisema kuwa upatanisho huo anaousimamia una baraka za Mungu na amemtia moyo wa kuendelea kusimamia maridhiano kwani ni afya ya Taifa.

Aidha, amemshukuru Rais pamoja na  viongozi mbalimbali wa Serikali waliochangia ujenzi wa Kanisa Kuu la KKKT, Dayosisi ya Karagwe pamoja na waumini na wadau mbalimbali.

Pia, Askofu Bagonza ametoa pole kwa Serikali na Watanzania  kufuatia vifo na majeruhi vilivyotokana na janga la kiasili wilayani Hanang, mkoani Manyara.

Dayosisi ya Karagwe ilizinduliwa mwaka 1979 ambapo ujenzi wa Kanisa hilo kuu ulianza Februari 24, 2023 na kukamilika Novemba 2023. Ujenzi wa Kanisa hilo umegharimu Sh400 milioni