Rais Samia afanya teuzi za washauri wake

Muktasari:
- Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kwa kuwateua washauri wawili wa Rais katika masuala ya sheria na mabadiliko ya tabianchi na mazingira.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya teuzi mbili akiwateua washauri wawili wa Rais katika masuala ya sheria na mabadiliko ya tabia nchi na Mazingira.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu leo Ijumaa Aprili 21, 2023 Rais Samia amemteua Jaji George Masaju kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.
Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Novemba5, 2015 hadi Februali 2018 kipindi cha utawala wa Rais wa awamu ya tano John Magufuli.
Kwa mujibu iliyotolewa uteuzi wake umeanza jana Alhamisi Aprili 20, 2023.
Pia Rais Samia amemteua Dk Richard Muyungi kuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira.
Kabla ya uteuzi huo Dk Muyungi alikuwa meneja wa Mazingira katika shirika la umeme (Tanesco), pia aliwahi kuwa mkurugenzi wa mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa awamu ya tano.
Uteuzi wa Dk Muyungi umeanza tangu Jumatano Aprili 19, mwaka huu.